Wednesday , 8 February 2023
Home Kitengo Michezo Alichoandika Mo Dewji kifo cha Hanspope
Michezo

Alichoandika Mo Dewji kifo cha Hanspope

Spread the love

 

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu ya Simba ya Dar es Salaam nchini Tanzania, Mohamed Dewji “Mo Dewji” amesema ni vigumu kukubali kwamba Zakaria Hans Pope amefariki dunia. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Hans Pope, aliyekuwa mjumbe wa bodi ya Simba na mwenyekiti wa kamati ya usajili wa timu hiyo, alifarini dunia usiku wa jana Ijumaa tarehe 10 Septemba 2021, katika Hospitali ya Agha Khan jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.

Dewji ambaye pia ni mwekezaji ndani ya mabingwa hao mara nne mfululizo wa ligi kuu Tanzania Bara, ameweka picha aliyopita yeye na Hans Pope huku akisema;

“Moyo wangu una maumivu makali sana. Bado ni vigumu kukubali kwamba Mjumbe wetu wa bodi Zakaria Hans Poppe hatunaye tena.

Pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na Wanasimba kwa ujumla kwa msiba huu mzito. Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yake mahali pema peponi.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Spread the love  MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida...

error: Content is protected !!