Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Iddi Azzan: Nilitaka kujiua
Habari za Siasa

Iddi Azzan: Nilitaka kujiua

Spread the love

KASHFA ya dawa za kulevya niliyobebeshwa, ilitaka kunipelekea kufanya uamuzi wa kujitoa roho. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Ni kauli ya Iddi Azzani, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kinondoni kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), alipozungumza na MwanaHALISI Online.

Tuhuma za Azzan kujihusisha na dawa za kulevya, ziliibuka mwaka 2013 na miaka miwili baadaye, tuhuma hizo zilishika hatamu wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu 2015, yeye akiwa miongoni mwa wagombea wa Jimbo la Kinondoni.

“Tuhuma hizo ziliniathiri sana pamoja na familia yangu, hasa watu niliokuwa nawaongoza, zilitoka mwaka 2013, baadhi ya mitandao na magazeti yalitumika kuandika tuhuma hizo, na zilizidi mwaka 2015. Kwa kweli zimeniathiri sana kisaikolojia mpaka sasa.

“Nilifikia mahali pabaya, jinsi nilivyo na heshima niliyonayo na audilifu wangu, halafu jambo hilo linatoka na linalazimishwa lionekane ni kweli, ilifika mahali nilisema bora nife, bora nijipige risasi nife ila familia yangu ilifanya kazi ya ziada,” amesema Azzan.

Pia mwaka 2017, Paul Makonda ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam alipoanza kampeni ya kutokomeza biashara ya uuzaji, usambazaji na utumiaji wa dawa za kulevya, jina la Azzan lilikuwa miongoni mwayo.

“Ningeshangaa kama nisingetajwa. Niliitwa polisi kuhusu tuhuma hizo, nilikaa siku nne huku uchunguzi ukifanywa kuthibitisha kama nahusika ama la! Baada ya siku nne niliachwa kwa kuwa hawakuona chochote kinachonihusisha na tuhuma hizo,” amesema.

“Na mimi nigeshangaa sana Makonda kama angetaja watu wote halafu mimi asinitaje, ningeona ni adui yangu. Kwa bahati nzuri naye akanitaja na nilitii amri yake ya kwenda polisi, sikwenda na wanasheria wala ndugu yanu,” amesema Azzan.

Azan amesema, alitumia nguvu nyingi kujisafisha dhidi ya tuhuma hizo, licha ya kwamba katika hali ya kawaida, zimeacha kovu, kwa kuwa tuhuma huwa hazifutiki.

Katika harakati zake za kujisafisha, Azzan amesema alijisalimisha polisi na hata kwenda katika Shirika la Polisi la Kimaraifa (Interpol), ili wachunguze juu ya tuhuma hizo, kwa minajili ya kumchukulia hatua kama anahusika au kumsafisha kama ahusiki nazo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!