Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari Hii hapa orodha ya vijana 470 waliochaguliwa kujiunga na Idara ya Uhamiaji Tanzania
Habari

Hii hapa orodha ya vijana 470 waliochaguliwa kujiunga na Idara ya Uhamiaji Tanzania

Kamishna Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Dk. Anna Makakala
Spread the love

 

KAMISHNA Jenerali wa Uhamiaji Tanzania, CGI Dk. Anna Makakala amewatangazia vijana ambao wamechaguliwa kujiunga na Idara ya Uhamiaji kwa cheo cha Konstebo kuripoti Chuo cha Uhamiaji kilichopo Boma Kichakamiba Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)

Vijana hao wametakiwa kuripoti siku ya tarehe 19 Februari, 2022 kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 8:00 mchana.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 12 Februari, 2022 na Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, SI Paul Msele imefafanua kuwa, vijana hao wanapaswa kila mmoja afike na mashuka mawili yenye rangi ya bluu bahari, mto mmoja na foronya mbili za bluu bahari zisizo na maua.

Pia wanapaswa kufika na chandarua cha rangi ya bluu, madaftari makubwa 10, ndoo ya plastiki lita 20, fulana mbili za rangi ya dark bluu zenye shingo ya duara zisizo na mchoro wala picha, viatu vya raba na nguo za michezo (tracksuit, bukta na fulana), viatu vya mvua (rainboot), nguo chache nadhifu na za heshima.

Vitu vingine ni kadi ya bima ya afya au fedha shilingi 50,000 kwa wasio na bima ya afya, shilingi 20,000 ka ajili ya kupima afya, shilingi 60,000 ya kununua godoro na fedha za matumizi binafsi. Gharama za usafiri kutoka nyumbani kwenda Tanga Kichakamiba pia zitagharamiwa na mhusika mwenyewe.

Aidha, kila mmoja ametakiwa kufika na vyeti halisi vya elimu, kuzaliwa, JKT/JKU, Kitambulisho cha Taifa (NIDA) pamoja na picha tatu za pasipoti za hivi karibuni.

Ifuatayo ni orodha ya majina hayo hapa chini;

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

ElimuHabari

CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi

Spread the loveNAIBU Spika Musa Azzan Zungu amekipongeza Chuo cha Elimu ya...

HabariTangulizi

Dk. Slaa, Mwabukusi kuhojiwa na jeshi la Polisi Mbeya

Spread the loveJESHI la Polisi jijini Mbeya, linawashikilia kwa mahojiano Dk. Wilbroad...

HabariHabari Mchanganyiko

Kairuki Hospital Green IVF  yawanoa madaktari kuhusu upandikizaji mimba

Spread the love KITUO cha Upandikizaji Mimba cha Kairuki Hospital Green IVF...

error: Content is protected !!