Sunday , 29 January 2023
Home Kitengo Maisha Afya GGML yatoa milioni 84 mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI
Afya

GGML yatoa milioni 84 mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI

Spread the love

KAMPUNI ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imechangia zaidi ya Sh milioni 84 kusaidia mipango ya serikali katika mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani yaliyofanyika kitaifa jijini Mbeya. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mbeya … (endelea)

GGML na Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), kupitia Kampeni ya Kilimanjaro Challenge, wanashirikiana kwa namna mbalimbali ikiwamo kuongeza uelewa kuhusu janga la VVU na UKIMWI ili siku moja Tanzania itangazwe kuwa imetokomeza kabisa janga hilo katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.

Akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani juzi jijini Mbeya, Makamu wa Rais wa GGML anayeshughulikia miradi endelevu, Simon Shayo alisema kaulimbiu ya mwaka huu isemayo “Zingatia Usawa, Tokomeza Ukimwi, Tokomeza magonjwa ya mlipuko,” ni muhimu kwa jamii ya Geita na Tanzania kwa ujumla.

Alisema mpango wa GGML Kili Challenge ni mradi mahsusi kutoka katika sekta binafsi ambao umeisaidia serikali kwa zaidi ya miaka 20 katika mapambano dhidi ya VVU.

“Kupitia mpango huu, wachangiaji wenzetu wameendelea kuwa mstari wa mbele kudhibiti janga la VVU kwa kuhakikisha utoaji huduma za kimatibabu unazingatia utu na haki za wale wote wanaoweka imani yao kwetu hususani wale walio hatarini zaidi.

“Tunaziomba sekta binafsi nchini kuungana na GGML na kusaidia mfuko wa Ukimwi ili kuwezesha mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI kuwa endelevu. Bila kuwa na mipango imara ya kuhakikisha usawa katika utoaji wa huduma hizi za kimatibabu ni dhahiri duniani itashindwa kufikia lengo lake la kutokomeza Ukimwi ifikapo mwaka 2030” alisema.

Kama raia anayewajibika, GGML pia iliandaa kampeni ya upimaji wa VVU kwa hiari kwa wiki mbili ikilenga kufikia asilimia 80 ya wafanyakazi wake 5000. Hao ni wafanyakazi walioajiriwa moja kwa moja na wakandarasi.

Shayo aliongeza kuwa maendeleo chanya ya kijamii na kiuchumi ya mkoa na nchi yetu ni matokeo ya jamii yenye afya.

“GGML ni kampuni inayothamini mali na watu wake. GGML inaamini kuwa uwekezaji unaofaa katika afya ya wafanyakazi utaleta nguvu kazi yenye afya na kuongeza tija katika utendaji na ukuajiji wa kibiashara,” alisema Shayo.

Alisema kuanzia tarehe 1 – 14 Desemba 2021, GGML imealika jumla ya washauri nasaha 15 waliopata mafunzo ya UKIMWI kutoka serikalini na hospitali binafsi kufanya Upimaji wa VVU kwa hiari katika eneo lote la Mgodi.

“Ikiwa na wafanyakazi walioajiriwa na wakandarasi zaidi ya 5,000, GGML inawakilisha sehemu kubwa ya jamii ya Mji wa Geita ambao kama wakiwa wameelimishwa vya kutosha kuhusu VVU na UKIMWI, watakuwa na ushawishi chanya miongoni mwa jamii nzima ya Geita.

GGML Kilimanjaro Challenge dhidi ya VVU & UKIMWI ilizinduliwa zaidi ya miaka 20 iliyopita kwa lengo la kuongeza uelewa wa janga hili na kutoa msaada wa kifedha kwa mipango ya VVU na UKIMWI.

Tangu kampeni ya GGML Kilimanjaro Challenge ilizinduliwe miaka 20 iliyopita, zaidi ya  watu 800 kutoka sehemu mbalimbali dunia wameshiriki kwa kupanda Mlima Kilinjaro kwa njia ya kawaida na kuuzunguka mlima kwa kutumia baiskeli.

Kilimanjaro Challenge imebadilika na kushirikisha makampuni ya ndani na nje ya nchi na watu binafsi kutoka duniani kote hali iliyosaidia kuchangisha zaidi ya Sh bilioni 1.3 tangu 2018 kwa ajili ya miradi ya kinga, matunzo na matibabu ya VVU nchini kote.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Afya

JK atoa ya moyoni kuhusu huduma za afya

Spread the love  RAIS Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete amesema huduma za afya...

AfyaHabari za Siasa

Heche amvaa Ummy Mwalimu kisa bima ya afya

Spread the love  MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chadema, John Heche amemtaka...

Afya

Asilimia 86 wenye umri zaidi ya miaka 18 wapata dozi kamili ya Uviko-19

Spread the love  KWA kipindi cha miezi sita kuanzia mwezi Julai hadi...

Afya

Waziri anusa ufisadi matumizi fedha za UVIKO-19

Spread the love  NAIBU Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel, ameagiza uchunguzi...

error: Content is protected !!