Wednesday , 8 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Tanzania yaamriwa ilimpe mamilioni Mtanzania iliyomvua uraia
Habari Mchanganyiko

Tanzania yaamriwa ilimpe mamilioni Mtanzania iliyomvua uraia

Spread the love

 

MAHAKAMA ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR), imeamuru Serikali ya Tanzania, imlipe fidia ya zaidi ya  Sh. 50 milioni, Mtanzania Anudo Ochieng Anudo, kutokana na hasara aliyoipata baada ya kufukuzwa nchini kinyume cha sheria. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Hukumu hiyo imetolewa na Makamu wa Rais wa AfCHPR, leo Alhamisi, tarehe 2 Desemba 2021, katika kikao chake cha kawaida cha 63, kilichofanyika jijini Dar es Salaam.

Katika hukumu hiyo, Serikali ya Tanzania imemriwa kumlipa Anudo kiasi hicho cha fedha, kama fidia dhidi ya hasara aliyoipata baada ya kupelekwa nchini Kenya kwa nguvu Mei 2018, akidai sio Mtanzania.

Katika fedha hizo, Sh. 10 milioni ilikuwa ni fidia dhidi ya hasara aliyoipata kwa kushindwa kuendesha biashara zake zilizokuwa nchini, Sh. 50 milioni fidia kwa wana familia yake, wakiwemo watoto na wazazi wake.

Ambapo watoto wake wanne kila mmoja atapata Sh. 10 milioni na wazazi wake kila mmoja atapata Sh. 5,000,000.

Pia, Serikali ya Tanzania imetakiwa kumruhusu Anudo kuingia nchini Tanzania.

Katika hukumu hiyo, AfCHPR, imeiamuru Serikali ya Tanzania kurekebisha sheria zake, ili kutoa nafasi kwa watu wanaokabiliwa na changamotro za uraia.

Serikali ya Tanzania imeamriwa kutekelza hukumu hiyo ndani ya miezi sita tangu tarehe ya kutokewa kwa hukumu hiyo.

Anudo aliyejitambulisha kwamba amezaliwa 1979 wilayani Butiama mkoa wa Mara, nchini Tanzania, alifungua kesi dhidi ya Serikali ya Tanzania, akipinga kuvuliwa uraia na kufukuzwa nchini.

Anudo alidai kuwa, 2012 alipoingia Tanzania, kwa ajili ya kushughulikia masuala ya ndoa yake, alipokonywa hati yake ya kusafiria Passport na katika Kituo cha Polisi Wilaya ya Bababati.

Alidai, baadae alivuliwa uraia wake na kupelekwa nchini Kenya ambako nako walimkataa na kumrudisha nchini, lakini aliishia kuwa mtu asiye na ardhi kati ya mpaka wa Tanzania na Kenya ulioko Sirari.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mawakili waiburuza mahakamani TLS, EALS

Spread the love  WAKILI Hekima Mwasipu na wenzake wawili, wamefungua kesi katika...

Habari Mchanganyiko

Uvuvi bahari kuu wapaisha pato la Taifa

Spread the love  SERIKALI imesema uvuvi wa bahari kuu umeliingizia Taifa pato...

Habari Mchanganyiko

DPP aweka pingamizi kesi ya ‘watu wasiojulikana’

Spread the love  MKURUGENZI wa Mashtaka nchini (DPP), ameweka pingamizi dhidi ya...

Habari Mchanganyiko

Washindi saba safarini Dubai NMB MastaBata ‘Kote Kote’

Spread the loveKAMPENI ya kuhamasisha matumizi ya Mastercard na QR Code ‘Lipa...

error: Content is protected !!