April 14, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Futeni vyama vya upinzani – JPM ashauriwa

Rais John Magufuli

Spread the love

KAMA Chama Cha Mapinduzi (CCM), kinaamini kwamba kina haki kuliko vyama vingine ndani ya nchi hii, basi upelekwe muswada bungeni ili vyama vya upinzani vifutwe. Anaripoti Dandon Kaijage, Dodoma … (endelea).

Akizungumza na wanahabari jijini Dodoma leo 12 Novemba 2019, Mwenyekiti wa Kijiji cha Mtungumo, Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma, Juma Lubeleje (Chadema) amesema, kwa mazingira ya sasa, kuna kila sababu nchi iamue kufuta vyama vya upinzani.

Amesema, unyanyasaji kwa vyama vya upinzani umedhihiri wakati wa uchukuaji na urejeshaji fomu za kugombea nafasi mbalimbali, kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.

Lubeleje amesema, mbaya zaidi ukiukwaji wa sheria unafanywa na Jeshi la Polisi kwa kuwapiga na kuwakamata wapinzani kwa maslahi ya chama tawala.

“Tumeona wakati wa kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali katika serikali za mitaa, hivi kweli inaingia akilini kuwa wagombea wa upinzania hawajui kujaza fomu au hawajui kuandika? ni kweli CCM pekee ndio wanaoweza kujaza fomu viruzi tu.

“Lakini pia tumeshuhudia watendaji wakikimbia ofisi zao kwa lengo la kukwepa kupokea fomu za wagombea, na kufikia hatua ya kujifungia ndani jambo kama hilo likiendelea bila kukemewa, linaweza kuzua machafuko,” amesema Lubelege.

Ameshauri, ikiwa CCM wanadhani nchi hii ipo kwa ajili yao, basi upelekwe muswada bungeni ili kufuta vyama vya upinzani nchini.

error: Content is protected !!