Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kumbe Mkapa ndio injinia wa Magufuli!
Habari za Siasa

Kumbe Mkapa ndio injinia wa Magufuli!

Spread the love

MCHANGO wa Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa una nafasi kubwa katika kumwezesha Dk. John Magufuli kuwa rais wa Tanzania. Anaripoti Martin Kamote … (endelea).

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitabu cha Maisha ya Rais Mkapa kiitwacho ‘Maisha Yangu, Kusudio Langu’ leo tarehe 12 Novemba 2019, Rais Magufuli amesema, hata alipotaka kugombea urais, alikwenda kwa rais huyo mstaafu.

Rais Magufuli alianza kuzungumzia safari yake ya kisiasa tangu alipoanza kugombea ubunge kwa mara ya kwanza mwaka 1995, katika jimbo la Biharamuro Mashariki (sasa Chato).

“Nakumbuka siku hiyo mbele ya umati mkubwa wa watu, Mzee Mkapa alinishika mkono wangu juu na kuwaambia wananchi ‘nileteeni kijana huyu,’ amesema na kuongeza;

“Najua baadhi yenu mtakumbuka picha niliyopiga wakati huo, nilikuwa na nywele nyeusi, kipara hakikuwepo, kichwa changu bado kilikuwa safi, lakini huo mwaka 1995, mzee huyu ndiye aliyeniinua, sikujua kwanini aliniinua,” amesema na kuongeza;

“Lakini Mzee Mkapa hakuishia hapo, baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge, alinichagua kuwa waziri wa Wizara ya Ujenzi, chini ya mama Anna Abdallah.

“Mpaka sasa bado najiuliza, nini kilimsukuma kunichagua kuwa naibu waziri. Nikiwa naibu waziri, Mzee Mkapa alinisaidia kinijengea kujiamini na ujasiri.”

Amesema, kulikuwa na tabia kwa makatibu wakuu kutoheshimu manaibu waziri, lakini Mzee Mkapa alisaidia maagizo yake (Rais Magufuli) kutekelezwa.

“….lakini mimi nikiwa Naibu Waziri, Mzee Mkapa alinijengea ujasiri mkubwa sana, nilikuwa nikimpa maelezo Katibu Mkuu, akikataa kutekeleza, Mzee Mkapa alikuwa akitoa maelekezo ya kutekeleza.

“Hii ilinifanya nifahamu kuwa, kwa Mzee Mkapa wateule wake wote ni sawa. Hakuna mkubwa wala mdogo, la msingi ufanye kazi. Kingine nilichojifunza kwake, akikueleza jambo au ukimshauri jambo, akalikubali na likiharibika hakuachi peke yako,” amesema.

Ametoa mfano kwa baadhi ya mapendekezo yake jinsi yalivyogonga mwamba, lakini Mzee Mkapa alisaidia kuyasukuma na kutekelezwa.

“Wakati nikiwa Waziri wa Ujenzi, nilipowasilisha nyaraka katika Baraza la Mawaziri, kupendekeza ushauri kwa serikali kutenga shilingi bilioni1.85 kila mwezi, za kujenga barabara, mawaziri wengi walinipinga.

“Lakini licha ya mawaziri wengi kupinga, alisimamia na akaelekeza utekelezaji wa waraka huo. Aliniambia waziri endelea na akamwambia Mzee Mramba (Basil Mramba), aanze kutenga kiasi hicho cha fedha za kujenga barabara kwa nguvu zetu wenyewe,” amesema.

Na kwamba, uamuzi huu ndio ukawa ufunguo wa kuanza kutengeneza barabara na madaraja mengi nchini.

“Watanzania hatuna budi kumshukuru Mzee Mkapa kwa uamuzi wake huu wa kishujaa, uliotufanya Watanzania kuanza kujenga barabara zetu kwa kutumia fedha zetu wenyewe,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!