Wednesday , 8 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Dk. Ndumbaro aeleza umuhimu wa Chama cha Mawakili wa Serikali
Habari Mchanganyiko

Dk. Ndumbaro aeleza umuhimu wa Chama cha Mawakili wa Serikali

Spread the love

Waziri wa Katiba na Sheria, Damas Ndumbaro, ameeleza umuhimu wa Chama cha Mawakili wa Serikali kwa kueleza majukumu yao kuwa mazito na muhimu kwa serikali. Anaripoti Urumasalu Kisung’uda, TUDARCo … (endelea)

Katika Mkutano Mkuu wa Chama cha Mawakili wa Serikali tarehe 29 Septemba 2022 Mkoani Dodoma wenye lengo la kuzindua Chama cha mawakili Ndumbalo amesema Wanasheria wanahusika na utoaji haki, usimamizi wa sheria, tafsiri za sheria, kusuluhisha migogoro katika kutia sahihi na mikataba.

Amesema chama hicho kitashughulika na masuala ya kitaaluma , maadili ya wanasheria kwa kutoa changamoto za kimaadili zinazowakabili.

“Pia chama hiki cha mawakili kinatarajiwa kuleta umoja wenye nguvu na jukwaa mahususi la kushauri Serikali katika kazi zake, vilevile jukwaa hilo litakuwa sehemu ya majadiliano kati ya wanasheria kwa Serikali ambayo haikuwepo kabla,” amesema Ndumbaro.

Ndumbalo amesema chama hiki kitakuwa eneo la kuwasilisha mawazo ya wanachama yanayoathiri taaluma yao kwa namna moja au nyingine.

“Chama hiki ni sehemu ya kuimarisha mfumo wa sheria ambao unaathiri sekta ya sheria katika utumishi wa umma, pia utasimamia na kuendesha mafunzo mbalimbali ya mawakili walioko katika utumishi wa umma,” amesema Ndumbaro.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoMichezo

Kengold wakabidhiwa kombe NBC Championship

Spread the loveMdhamini mkuu wa Ligi Daraja la Kwanza (NBC Championship) Benki...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

error: Content is protected !!