Friday , 29 September 2023
Home Kitengo Michezo Dk Mpango mgeni rasmi tamasha la washairi
Michezo

Dk Mpango mgeni rasmi tamasha la washairi

Makamu wa Rais wa Dk. Philip Mpango
Spread the love

MAKAMU wa Rais, Dk Philip Mpango anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye ufungaji wa tamasha la ushairi lililoandaliwa na Taasisi ya Usanifu wa Kiswahili na Ushairi Tanzania (UKUTA) kwa kushirikiana na Chama cha Kuendeleza Washairi Zanzibar (CHAKUWAZA) linalotarajia kuanza Julai 27 hadi 29 kwenye Chuo Kikuu kishiriki cha Elimu (DUCE) jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Huku ufunguzi wa tamasha hilo utafanywa na Makamu wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za UKUTA, Katibu Mkuu wa chama hicho, Hassan Ligile alisema tamasha hilo litasindikizwa na matukio mbalimbali yakiwemo ngonjera, mashairi, taarab asilia, kwaya, bendi, na ngoma ya Msewe.

Tukio lingine ni igizo la Kifimbo cheza ambalo litasisitiza matumizi sahihi ya lugha ya Kiswahili.

Ligile alisema kutakuwa na mada mbalimbali kama umuhimu na malengo ya UKUTA na CHAKUWAZA huku jambo lingine litajadili kuhusu kwamba Kiswahili kinafaa kufundishia na la tatu ni je Kiswahili kina misamiati ya kutosha.

Hassan Ligile

Katika tamasha hilo kutakuwa na mada ya mwanamke na maendeleo sambamba na kupinga ukatili na unyanyasaji wa kijinsia.

Ligile alisema siku tatu kabla ya tamasha hilo uongozi wa UKUTA na CHAKUWAZA watashiriki shughuli mbalimbali za kijamii.
Alisema katika tamasha hilo pia kutakuwa na uzinduzi wa vitabu vya Ushairi.

Aidha katika tamasha hilo wamezialika nchi za Kenya, Uganda na Rwanda huku mikoa mitano ya Morogoro, Tanga, Pwani, Arusha na Mtwara itakuwa sehemu ya ushiriki.

Ligile alisema wamezialika sekondari mbalimbali zilizoko Manispaa ya Temeke sambamba na Vyuo Vikuu vya Dodoma (UDOM), Chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro (MUM), Chuo Kikuu Zanzibar na vinginevyo.
Ligile aliitaja kauli mbiu ya tamasha hilo ni Ushairi ni biashara huku akitoa wito kwa wadau mbalimbali wa sanaa kujitokeza kwa wingi ili kujipatia ladha mbalimbali za ushairi kutoka kwa malenga kama Mrisho Mpoto ‘Mjomba’ na wengineo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Meridianbet yaibukia Tandika, yafungua duka jipya

Spread the love BAADA ya kupita maeneo mbalimbali hatimae kampuni yaMeridianbet imeibukia...

BiasharaMichezo

Ukiwa na Meridianbet ni rahisi kuwa milionea

Spread the love  CARABAO Cup raundi ya 3 Uingereza inaendelea na mechi...

Michezo

Jezi ya Samatta iliyoifunga Liverpool kuuzwa Genk

Spread the love  KLABU ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji imeamua kuanza...

BiasharaMichezo

Hii ndio historia ya El-Clasico, derby bora zaidi duniani

Spread the love  KILA nchi ina vilabu viwili hasimu na pinzani nje...

error: Content is protected !!