MFANYABIASHARA maarufu nchini Tanzania, Rostam Aziz, ameomba radhi kufuatia kauli yake iliyodai kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, haiko huru kutokana na baadhi ya mahakimu wake kuendesha kesi kwa kufuatia maelekezo kutoka serikalini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).
Akizungumza na waandishi wa habari jini Dar es Salaam, leo Jumanne, Rostam amedai kauli hiyo aliitoa kwa kuteleza.
Mfanyabiashara hiyo ameomba radhi baada ya Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania (JMAT), kumtaka aombe radhi au athibitishe tuhuma zake kama ni kweli.
“Nimesoma taarifa ya chama cha majaji na Mahakimu, ningependa kuwahakikishia Umma kwamba wakati nazungumzia kuhusu uwekezaji wangu halikuwa kusudi langu kudharau mahakama zetu. Nilimaanisha mahakama zetu ziendane na kiwango cha kimataifa kuheshimu uwekezaji. Hivyo niliteleza,” amesema Rostam.
JMAT ilitoa wito kwa Rostam aombe radhi, Leo tarehe 4 Julai 2023, kupitia tangazo lake ililitoa kwenye gazeti la The Citizens.
Kupitia tangazo hilo, JMAT imesema halijawahi kupokea tuhuma au lalamiko lolote kutoka kwa mtu kuonyesha afisa wa Mahakama kupigiwa simu na kuelekezwa namna ya kutoa maamuzi katika Mahakama hiyo.
Tangazo hilo limesema, Mahakama ni chombo pekee cha utoaji haki nchini kwa mujibu wa Katiba na huendesha shughuli zake kwa uhuru bila kuingiliwa na mtu au chombo chochote.
JMAT kimesema kauli iliyotolewa na Rostam inahatarisha uhusiano na ushirikiano katika mihimili mitatu ya dola ndani ya nchi.
Leave a comment