Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Mpango awataka wakimbiza Mwenge kufichua ubadhirifu
Habari za Siasa

Dk. Mpango awataka wakimbiza Mwenge kufichua ubadhirifu

Dk Philip Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Spread the love

 

MAKAMU wa Rais Dk. Philip Mpango amewataka viongozi wa kukimbiza Mwenge wa Uhuru kuhakikisha miradi inayozinduliwa inaendana na thamani ya fedha zilizotumika. Anaripoti Mwandishi Wetu, Njombe … (endelea)

Wito huo ameutoa leo Jumamosi tarehe 2 Aprili 2022 katika uzinduzi wa Mwenge wa Uhuru Kitaifa uliofanyikia mkoani Njombe.

Dk. Mapango amewataka vijana hao ambao wapo sita kwa idadi, kuhakikisha kuwa wanaripoti kwenye vyombo vya sheria miradi yote watakayoitilia mashaka ili wahusika wachukuliwe hatua zaidi.

Aidha ameitaka Takukuru ikamilishe uchunguzi wa miradi 52 iliyotiliwa shaka katika mbio za mwenge za mwaka jana “na kama kuna ushahidi wa kutosha muwafikishe kwenye vyombo vya sheria.”

Amesema kupitia mbio za Mwenge mwaka huu Taifa lina wajibu wa kupambana na rushwa chini ya kauli mbiu isemayo ‘Kupambana na Rushwa ni Jukumu Langu’ “kila mtu anapaswa kuacha kutoa au kupokea rushwa.”

Pia Dk. Mpango alisisitiza umuhimu wa kuchukua tahathari za ugonjwa wa Ukimwi kwani licha ya kupungua lakini bado maambukizi ni mengi.

“Pamoja na UKIMWI kuendelea kuwepo maambukizi mapya yameshuka kutoka 110,000 mwaka 2010 hadi maambukizi 68,000 mwaka 2020. Bado ni wengi mno.”

Vile vile alisema maambukizi ya mama kwenda kwa mtoto yameshuka kutoka asilimia 18 mwaka 2010 hadi asimilia 7 mwaka 2020.

Alibainisha kuwa utafiti wa mwisho wa viashiria na matokeo vya UKIMWI ngazi ya kaya uliofanyika mwaka 2016/17, ulionesha kuwa mikoa iliyokuwa na maambukizi ya juu ni Njombe asilimia 11.4, Iringa asilimia 11.3 na Mbeya asilimia 9.3.

“Hivi ni viwango ambavyo bado havikubaliki popote, tunapoteza nguvu kazi ya Taifa kwahiyo ni vyema kuendela kuchukua hatua za kujilinda na kufuta ushauri wa wataalamu,”

Dk. Mpango ametumia pia fursa hiyo kuhamasisha watu kujilinda dhidi ya malaria,kuepuka matumizi ya dawa za kulevya na kutunza mazingira.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Samia awataka watanzania kudumisha muungano

Spread the loveRais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendeleza Muungano kwa...

error: Content is protected !!