October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Mpango atoa somo Wimbo wa Taifa

Spread the love

MAKAMU wa Rais Dk. Philip Mpango amelazimika kuanza hotuba yake kwa kufundisha wananchi namna ya kusimama wakati wa kuimba Wimbo wa Taifa. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Dk. Mpango ametoa somo hilo kwa kile alichodai wakati wa kuimba wimbo wa Taifa ameshuhudia baadhi ya watu wakiwa wamesimama huku mikono ikiwa mifukoni na mwingine akiweka mikono nyuma.

Makamu huyo wa Rais akihutubia leo tarehe 17 Agosti, 2022, katika hafla ya kukabithi magari ya mradi wa kukuza utalii kusini (REGROW), alikatisha hotuba yake na kwenda pembeni mwa podiamu ambapo alionesha wananchi namna ya kusimama wakati wa kuimba wimbo wa Taifa.

Dk. Mpango amesimama wima na kubana mikono yake mbavuni ikiwa imenyooka kuelekea chini na kusema, “hivi ndiyo unapaswa kusimama mikono yako unaibana hapa (anaonesha kwa vitendo). Sasa kuna wengine walikuwa wameweka mikono mifukoni, mwingine kaweka nyuma. Hapana. Huo sio utaratibu na heshima kwa wimbo wa Taifa, naomba kuwasisitiza Watanzania wote kupitia hadhara hii tuziangatie utaratibu na heshima inayotakiwa kwa tunu yetu ya Taifa, wimbo wa taifa ndio unaotutambulisha.”

error: Content is protected !!