October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ruto: Machifu, watumishi ‘waliotekwa’ upinzani warejee kazini

Spread the love

RAIS mteule w Kenya, Dk. William Ruto amewataka machifu na watumishi wa umma waliokuwa wanatumiwa na wanasiasa kuwafanyia kampeni, warejee kazini ili watekeleza majukumu yao.

Dk. Ruto ameidai baadhi ya machifu wamekuwa mateka wa mrengo fulani wa kisiasa, kuutafutia kura. Inaripoti Mitandao ya KImataifa… (endelea)

Amesema watumishi wa umma hawapaswi kushiriki siasa na badala yake wanatakiwa kuhudumia umma.

Ruto ametoa kauli hiyo leo tarehe 17 Agosti, 2022 katika Kauti ya Karen, jijini Nairobi nchini humo wakati akihutubia wajumbe waliochaguliwa kupitia vyama tanzu vya Umoja wa Kenya Kwanza ambao umefanikiwa kumpa ushindi katika nafasi ya urais dhidi ya mpinzani wake wa karibu Raila Odinga.

 

Amesisitiza watumishi wa umma wanapaswa kutekeleza wajibu wao bila kuegemea upande wowote wa kisiasa.

“Kwa waliotumika kisiasa hasa machifu, warejee kazini kutekeleza majukumu yao…Wakenya wanataka maendeleo… Watumishi wa umma tunatarajia mfanyie wananchi kazi bila mapendeleo,” ” amesema.

Wakati akifanya kampeni kusaka urais, Ruto alikuwa akilalamikia machifu na wakuu wa polisi kutumiwa na serikali kufanyia kampeni wapinzani wake.

Katika kinyang’anyiro cha urais tarehe 9 Agosti, 2022, Ruto alimenyana na kinara wa Azimio, Raila Odinga.

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), ilimtangaza rasmi kuwa mshindi. Odinga hata hivyo amepinga matokeo hayo.

Ruto amehudumu kama naibu wa rais kati ya 2013 – 2022, na amekuwa akidai kutengwa serikalini hasa baada ya Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa ODM, Odinga kutangaza kuzika tofauti zao za kisiasa 2018 kupitia salamu za maridhiano maarufu kama ‘Handisheki’.

“Siasa zitekelezwe na wanasiasa. Watumishi wa umma wafanye kazi zao,” amesema.

Dk. Ruto amewahakikishia waliokuwa wamezuiwa kurejea nchini humo kwa sababu za kisiasa, warejee bila hofu yoyote.

error: Content is protected !!