Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Morogoro yapokea bilioni 111 miradi ya maendeleo
Habari Mchanganyiko

Morogoro yapokea bilioni 111 miradi ya maendeleo

RC Morogoro
Spread the love

MKUU wa mkoa wa Morogoro, Fatuma Mwasa, amesema mkoa wa Morogoro umepokea kiasi cha Sh111.5 bilioni kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kwa ajili ya miradi ya maendeleo. Anaripoti Apaikunda Mosha, TUDARCo… (endelea).

Akizungumza leo Jumatano tarehe 17 Agosti, 2022 katika hafla ya kutoa magari ya mradi wa kuendeleza utalii kusini (REGROW), Mwasa amesema fedha hizo zililenga kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo miradi ya Afya, Elimu na Maji, ambapo kwa sasa imekamilika kwa 90 mpaka 100.

Mwasa amesema serikali imerudisha eneo la ardhi, ukubwa wa mashamba 9 ambayo wamegawanya katika maeneo ya kilimo, maeneo ya wafugaji, eneo kwa ajili ya matumizi ya taasisi za serikali na makazi ya wananchi.

Aidha, ameiomba serikali kurudisha mpango wa ujenzi wa barabara iliolenga kupita nje ya hifadhi yaani BYPASS kwani itasaidia kupunguza vifo vya wanyama vitokanavyo na ajali za magari kwani hifadhi inapoteza wastani wa mnyama mmoja kwa siku kutokana na ajali, “kati ya mwaka 2015 na 2021 idadi ya wanyama 1,889 waligogwa na magari,” amesema mkuu wa mkoa huyo.

Pia amesema itasaidia kupunguza takataka zinazotupwa na watumiaji wa barabara hiyo ikiwa ni wastani wa kilo 138 ambazo hutupwa barabarani kila siku ambapo kati ya mwaka 2015-2021 jumla ya kilo 14,956 za takataka zilitupwa hifadhini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Puma Energy Tz: Watanzania tudumishe amani kuvutia uwekezaji

Spread the loveKAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imewakutanisha wadau mbalimbali katika...

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

error: Content is protected !!