Tuesday , 5 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Mpango akiri Watanzania wengi bado maskini
Habari za SiasaTangulizi

Dk. Mpango akiri Watanzania wengi bado maskini

Spread the love

SIKU chache baada ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango kusoma Bajeti ya Kuu ta Tanzania kwa mwaka 2019/20, huku ikielezea ukuaji wa pato la Mtanzania kukua, lakini leo amekiri kuwa bado Watanzania ni maskini. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Dk. Mpango ametoa kauli hiyo ambayo imepingana na ripoti yake Bajeti aliyosoma Bungeni jijini Dodoma tarehe 13 Juni, 2019, alipokuwa anapokea gawio la hisa la Sh. 9.9 bilioni, kutoka kwa benki ya CRDB, ambayo asilimia 80 ya hisa zake zinamilikiwa na Watanzania wazawa.

Katika Bajeti ya 2019/20 imeeleza kuwa, pato la wastani la kila mtu kwa mwaka 2018 lilifikia Sh. 2.4 milioni (2,458,496), kutoka Sh. 2.3 (2, 327,395) mwaka 2017. Hii maana yake ni kuwa, pato la mtu mmoja mmoja kwa siku limeongezeka kutoka 6,376.4 mwaka 2017 hadi 6,735.6 2018.

Dk. Mpango amesema kuwa pamoja na kupokelewa kwa gawio hilo lakini bado watanzania wengi ni maskini na wanaishi katika maisha mabaya kwa kushindwa kupata mahitaji muhimu.

Amesema licha ya viongozi kujiona kuwa wao wanamaisha mazuri na kuvaa suti, lakini bado wapo Watanzania ambao wanakunywa maji machafu ambayo hayastahili kunywewa hata na mifugo.

Dk. Mpango amesema wapo wakina mama ambao wanashindwa kwenda kupata huduma ya kujifungua kutokana na kukosekana kwa hospitali, kuna sehemu kuna hali mbaya sana ya kiuchumi.

Waziri amesema umefika wakati ambao kila Mtanzania anapaswa kujenga utamaduni wa kujitegemea ikiwemo kununua hisa kwenye masoko ya hisa na mabenki kuliko kutegemea watu wa nje ndiyo wawekeze.

“Napongeza hatua CRDB kutoa kiasi cha Sh 9.9 bilioni kwa taasisi, halmashauri na vyama vya ushirika vyenye hisa katika benki hiyo,” amesema.

Amesema, kumekuwa na wizi katika mabenki jambo alilosema tayari ameagiza uchunguzi wa kina ufanyike ingawa hakuitaja benki ambayo inalalamikiwa na wateja kuhusu wizi huo ambao alisema unakatisha tamaa watu kuweka fedha zao.

Pia Dk. Mpango alibainisha kuwa umefika wakati wa mabenki kuwafuata wateja ikiwemo kupeleka magari ya huduma za benki minadani ambako watu wanauza mifugo halafu wanatembea na fedha nyingi badala ya kusubiri wateja wawafuate maofisini.

Sambamba na hilo alizungumzia alieleza namna wavyopata shida kubwa wakati wa majadiriano na mataifa kuhusu mikopo.

Alifafanua kuwa, wanapokwenda kukopa, majadiliano na watu katika masuala ya mikopo inakuwa shida, na kulazimika kuanza kuwaza katika mabadiriko.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa bodi ya CRDB, Ally Laay amesema Watanzania hawana utamaduni wa kuwekeza kwenye hisa jambo linalopelekea hisa nyingi kumikiwa na wageni na watu wachache.

Laay ameeleza kuwa hadi sasa Watanzania walionunua hisa kwenye soko la hisa hawazidi laki tano wakati fursa walizonazo ni nyingi kuweza kujitanua.

Alieleza kuwa asilimia 80 ya hisa za benki hiyo zinamikiwa na Watanzania wazawa na kuwa benki imekuwa imara zaidi kwa kujiimarisha maeneo yanayohitaji huduma ikiwemo kuongeza matawi.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Abdulmajidi Nsekela amesema wamejipanga vizuri kuhakikisha benki hiyo inakuwa ya mfano kwa nchi za usoni na sasa wanaajiri watumishi wenye weledi.

Mkurugenzi huyo, ameeleza mahusiano na wateja wao yamekuwa chachu ya mafanikio yao hata katika kutoa gawio kwa wanahisa wao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Baba yake Ole Sabaya ashinda Uenyekiti CCM – Arusha

Spread the loveLoy Thomas Sabaya ambaye ni Baba wa aliyekuwa Mkuu wa...

Habari za Siasa

Serikali yaagiza uchunguzi chanzo maporomoko Hanang

Spread the loveSERIKALI imeagiza uchunguzi ufanyike ili kubaini chanzo cha maporomoko ya...

Habari za SiasaTangulizi

Maafa Manyara: Rais Samia akatisha ziara yake Dubai

Spread the loveRAIS wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amekatisha ziara yake...

Habari za SiasaTangulizi

Wataalaam wa miamba watua Hanang

Spread the loveWaziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na...

error: Content is protected !!