Monday , 11 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Biteko: Tumsaidie Rais Samia kujenga nchi
Habari za Siasa

Dk. Biteko: Tumsaidie Rais Samia kujenga nchi

Spread the love

Ujumbe wa Marafiki waliosoma na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko ukiongozwa na Mbunge wa Hai, Saashisha Mafuwe umetoa pongezi kwa Dk. Biteko kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Wametoa pongezi hizo leo tarehe 3 Novemba 2023 katika ukumbi wa Bunge jijini Dodoma ikiwa ni pamoja na kumtakia heri katika majukumu yake mapya ambapo wamesisitiza kuunga mkono juhudi za Serikali.

Kwa upande wake, Dk. Biteko amewashukuru kwa kumtakia heri na kuwataka kufanya kazi kwa bidii ili azma ya Rais Samia itimie katika kujenga uchumi wa nchi na Watanzania wanufaike.

Ujumbe huo ni wanafunzi waliosoma Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine Mwanza (SAUT) na marafiki wengine waliosoma maeneo mbalimbali nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Biteko: Samia ni muumini wa maridhiano sio kwa kuigiza

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Mpango: Sitakufa bali nitaishi

Spread the loveMAKAMU  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk....

Habari za SiasaTangulizi

Mbowe: Miaka 62 ya uhuru tujenge upya mioyo yetu

Spread the loveWAKATI Tanganyika ikiadhimisha miaka 62 tangu kupata uhuru, Mwenyekiti wa...

Habari za Siasa

Rais Samia asamehe wafungwa 2,244

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewasamehe wafungwa 2,244, huku akiwabadilishia...

error: Content is protected !!