Thursday , 13 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge akerwa mawaziri “kuchati” bungeni, aomba mwongozo
Habari za SiasaTangulizi

Mbunge akerwa mawaziri “kuchati” bungeni, aomba mwongozo

Spread the love

MBUNGE wa Songwe, Philipo Mulugo, ameomba mwongozo bungeni jijini Dodoma, juu ya tabia ya baadhi ya mawaziri wanaodaiwa kutumia simu (kuchati na kuongea na simu), wakati wabunge wanaendelea kuchangia masuala ya msingi juu ya mustakabali wa nchi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Mulugo ameomba mwongozo huo leo tarehe 3 Novemba 2023, bungeni jijini Dodoma, wakati Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara anatoa mchango wake kuhusu taarifa za kamati za kudumu za Bunge, juu ya ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 2022.

Mbunge huyo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), amedai wakati Waitara anatoa mchango wake, baadhi ya mawaziri walikuwa wanachati kama anayoyazungumza hayawahusu.

“Mheshimiwa mwenyekiti, kama mbunge wa CCM moyo unaniuma mbunge mwenzetu anapochangia taarifa kama hii, inauma kuona wanaohusika mawaziri wanachati na simu, wanaongea na simu hawajali kile ambacho anakiongea Waitara. Kama vile jambo linapita, haomba mwongozo wako,” amesema Mulugo.

Baada ya Mulugo kutoa ombi hilo, Mwenyekiti wa Bunge, Daniel Sillo, alisema mwongozo kuhusu suala hilo utatolewa baada ya kikao hicho kuisha.

Wakati waitara anachangia, alitaka sheria itungwe ili kuwanyonga watu watakaobainika pasina shaka kuwa ni wezi wa mali za umma.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

IFP wakubali kuungana na ANC kuunda serikali

Spread the loveChama cha upinzani nchini Afrika Kusini, Inkatha Freedom Party (IFP)...

BiasharaHabari za Siasa

Prof. Mkumbo: Pato la taifa limefikia trilioni 148

Spread the loveWaziri wa Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema mwaka...

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

Deni la Serikali lafikia trilioni 91

Spread the loveWaziri wa Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo amesema hadi...

Habari za SiasaTangulizi

Mbunge Dk. Shogo Mlozi afariki dunia

Spread the loveMbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) ambaye pia ni...

error: Content is protected !!