Wednesday , 8 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chongolo: Hili la bandari wanataka kutupiga ‘break’
Habari za SiasaTangulizi

Chongolo: Hili la bandari wanataka kutupiga ‘break’

Spread the love

KATIBU Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo leo Jumamosi amesema upotoshaji unaofanywa na wanasiasa wa upinzani kuhusu uwekezaji katika bandari ya Dar es Salaam unalenga kuipiga ‘stop’ serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kutekeleza ilani ya chama hicho kwa ufanisi. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Amesema ikitokea CCM ikawasikiliza, wapinzani hao watapata hoja za kuwapiga ifikapo kipindi cha Uchaguzi Mkuu mwaka 2025.

Akizungumza katika mkutano wa chama hicho uliofanyika Kawe jijini Dar es Salaam, Chongolo amesema wakosoaji hao wamekosa hoja za kuikosoa serikali kwani katika sekta zote kama vile elimu, afya, miundombinu mambo yameenda vizuri.

“Barabara ya zilizobaki kama vile Kisarawe 2, Pemba mnazi na nyinginezo zikikamilika kwa upande wa Dar es salaam tutakuwa tunawawashia ‘indicator’ kubwa… wanataka kutupisha ‘break’ ili tusitende tuliyoazimia kwenye ilani yetu,” amesema.

Amesema dhamira ya CCM ni kuhakikisha Serikali inapata fedha za kutosha kutimiza malengo ya ilani ya chama hicho pamoja na kutatua changamoto za wananchi.

Amesema iwapo uwekezaji kenye bandari hiyo utafanyika, ni dhahiri kuwa fedha za utekelezaji wa ilani pamoja na changamoto nyingi za wananchi zitapatikana ndio maana wapinzani wamelenga kuwatoa kwenye mpango huo wa uwekezaji.

“Kwenye hili la bandari jamaa zetu wanajua tumewashika pabaya kwa sababu likitekelezwa mambo yetu yatakua na kasi ya ajabu, hatutakuwa tukifikiri namna ya kupata fedha ya kutatua changamoto za wananchi ndio maana wamechanganyikiwa …wanahaha,” amesema.

Chongolo amesema wakosoaji hao wa uwekezaji katika bandari ya Dar es Salaam kila waposema uongo, unajibiwa ndio maana wamepaniki na kuanza kutukana.

 

“Niwasihi wanaCCM msiwajibu kwa matusi, tuwajibu kwa vitendo…tuwaoneshe dhamana ya kuongozi nchi ina wajibu wa ukomavu, uvumilivu, wacheni tubebe wajibu wetu, tusibadilike kama wao.

“Sisi tusiingie kwenye kejeli, matusi yao na maneno yao ya kukatisha tamaa, tusonge mbele bila kukatishwa tamaa,” amesema.

Aidha, Chongolo amesema CCM itaendelea kuisimamia serikali ili itekeleze uwekezaji katika bandari hiyo huku ikisikiliza maoni ya wananchi.

“Kwa sababu wengine wanaita mkataba au makubaliano, ni hayohayo, kwani makubaliano ni mshahafu au Biblia kwamba haiwezi kubadilishwa? kama kuna mstari unaoweza kubadilishwa walete utumbukizwe!.

“Wakifanya hivyo, hapo masilahi ya nchi yatakuwa yamezingatiwa na matokeo yake utekelezaji wa ilani ya CCM na utatuzi wa changamoto za wananchi utafanyika kwa kasi,” amesema.

Aidha, ameshangaa kwanini wakosoaji hao hawataki kupeleka maoni yao kwa Serikali ili yafanyiwe kazi katika kuuboresha mkataba huo.

“Tutakuwa watu wa ajabu sana, tumepewa dhamana ya kuongoza nchi, tumeshika usukani, abiria anataka kushuka anatulazimisha kwani akishuka miguu yake si ndio itapata madhara?.

“Msiwe na mashaka wanaongalia kwa jicho moja wafungue yote mawili, tuliokalia kiti tunajua wajibu wetu,” amesema.

Wamebeba ajenda ya ubaguzi, wameanza kutubagua kwa maeneo, Mwalimu nyerere aliwahi kusema dhambi ya ubaguzi ni sawa na kula nyama ya mtu huwezi kuiacha.

Mbali na kueleza kusikitishwa na ajenda ya ubaguzi inayoenezwa na wapinzani hao, Chongolo amesema;

“Ukiona adui yako anakushangilia unapofanya jambo achana na hilo jambo halina nia njema, ukiona anapiga kelele unapofanya, hilo jambo lina tija… tusonge mbele,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia ni Mzanzibari: Shida Iko Wapi?

Spread the loveTAIFA linakabiliwa na upungufu wa fikra sahihi. Upungufu huu unaonekana...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mpina mwiba CCM, ahofia kuzibwa mdomo

Spread the loveWAKATI Chama cha Mapinduzi (CCM), kikijinasibu kuwa kinara wa demokrasia...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Mabeyo ametuepusha

Spread the loveNIMEGUSWA na uadilifu, utiifu na uaminifu wa Mkuu mstaafu wa...

Habari za SiasaTangulizi

CCM yaitaka TAKUKURU kuichunguza Chadema tuhuma alizoibua Lissu

Spread the loveCHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana...

error: Content is protected !!