July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Chongolo aagiza wanaCCM kushirikia vikao vya mashina

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo

Spread the love

 

KATIBU Mkuu wa chama tawala nchini Tanzania- Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amewataka wanachama wa chama hicho, kuhakikisha wanahudhuria vikao vya mashina. Anaripoti Mwandishi Wetu, Songwe … (endelea).

Amesema, kila mwana CCM ni mwanachama wa mashina na kwenye mashina ndiko kuliko na uhai wa chama hivyo ni lazima kila mmoja kuhakikisha anashiriki kikamilifu kwenye vikao vyote.

Chongolo alitoa maagizo hayo jana Jumapili, tarehe 11 Julai 2021, katika siku ya kwanza ya ziara yake Mkoa wa Mbeya akitokea mkoani Songwe, akiwa na wajumbe wa sekretarieti ya chama hicho.

Soma zaidi:-

Akiwa katika kikao cha mapokezi jijini Mbeya, Chongolo alisisitiza wanaCCM kuhudhuria vikao vya mashina ikiwa ndio msingi wa uimara wa Chama, na kila mwanachama anawajibika katika shina lake.

“Tumekuja huku chini kwenye Mashina kwa sababu huku ndipo kwenye uhai wa chama chetu, hapa kwenye shina tunazungumza na wanachama wote na ndipo penye wananchi,” alisema Chongolo

Aidha alisema “ukweli ni kwamba, sisi wote hapa ni wanachama wa Mashina, hapa hakuna mwanachama wa tawi, kata, wilaya, mkoa wala makao makuu, mwenyekiti wa chama chetu ni mwanachama wa Shina, mimi (Chongolo) ni mwanachama wa Shina, kila mmoja wetu hapa ni mwanachama wa Shina.”

Akiendelea na ziara katika wilaya ya Kyela, Chongolo alitembelea Shina namba 01 Tawi la Lema, shina namba 02 Tawi la Njisi, shina namba 02 tawi la Nazaleth ambapo ameeleza kwa undani umuhimu wa mikutano ya mashina.

“Tumekuja kuhimiza vikao hivi vya Mashina, kwetu sisi vikao hivi ni muhimu kuliko vikao vyote, kwa kiongozi yeyote mwakani anayetaka kugombea uongozi ndani ya chama lazima awe na muhtasari wa mahudhurio ya vikao vya mashina.”

Alisema “ukiwa mwanachama wa shina, ukaheshimu uongozi wa shina, ukamuheshimu balozi, tukajenga msingi wa kufuata kalenda ya chama chetu ya vikao, na tukashiriki kwa adabu huku tukimuheshimu mwenyekiti wa Shina chama chetu hiki hakitayumba milele.”

Katika hatua nyingine, Chongolo alitemmbelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo mradi wa ujenzi wa shule ya sekondari ya upili (High School) ya Lema a Ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa Kituo cha Huduma ya pamoja Mpakani katika eneo la Kasumulu mpakani mwa Tanzania na Malawi.

error: Content is protected !!