July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba Bingwa, mara nne mfululizo

Spread the love

 

MABAO mawili ya John Bocco na Chriss Mugalu yalitosha kuifanya Simba kutangazwa kuwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu wa 2020/21 kwenye mchezo.dhidi ya Coastal Union. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea)

Mchezo huo ulipigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam, kuanzia majira ya saa 1 usiku.

Baada ya kuchukua pointi tatu, sasa Simba itakuwa inafikisha alama 79, ambazo hazitafikiwa na timu yoyote kwenye msimamo wa Ligi.

Nafasi ya pili inashikiliwa na klabu ya Yanga, wenye pointi 70, hata wakishinda michezo yao miwili iliyosalia watafikisha pointi 76.

Huu utakuwa ubingwa wa nne mfululizo kwa klabu ya Simba toka msimu wa 2017/18, pia ubingwa huo utakuwa wa kwanza kwa kocha wa kikosi hiko Didier Gomes toka alipojiunga na klabu hiyo mwezi Januari.

Mabao ya leo ya Simba yalifungwa kwenye dakika ya 13 na Bocco, kupitia adhabu ndogo ya faulo na dakika 10 baade Mugalu alindika bao la pili na bao la 13 kwake kwa msimu huu, kwenye dakika ya 23

error: Content is protected !!