Monday , 4 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema yasogeza mbele maandamano Mwanza
Habari za SiasaTangulizi

Chadema yasogeza mbele maandamano Mwanza

Maandamano Chadema
Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesogeza mbele maandamano ya amani ya kupinga miswada ya sheria za uchaguzi na kudai katiba mpya, hadi tarehe 15 Februari 2024. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza, leo Alhamisi, Naibu Katibu Mkuu Chadema Bara, Benson Kigaila, amesema maandamano hayo yalipangwa kufanyika tarehe 13 Februari mwaka huu, kisha kufuatiwa na mkutano wa hadhara uliopangwa kufanyika Uwanja wa Furahisha jijini Mwanza.

Amesema baada ya Chadema kwenda kuomba kibali  katika Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela, ya kuutumia uwanja huo siku husika, walikosa kibali kwa maelezo kwamba tarehe waliyoomba kuna mtu mwingine aliomba na kupewa kibali cha kuutumia.

“Katibu mkuu alitangaza kwamba maandamano ya Jiji la Mwanza yatafanyika tarehe 13 Februari na ilipofika tarehe 5 katibu wa kanda na viongozi wa Jimbo la Ilemela walikwenda Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela kwa ajili ya kuomba kibali cha uwanja wa Furahisha kwa ajili ya mkutano sababu maandamano yataishia Furahisha ambapo waliambiwa tarehe 13 haina mtu mkurugenzi akakubali wapeni,” amesema Kigaila.

Kigaila amesema “tarehe 6 Februari walirudi wapate barua waliporudi wakaambiwa ile tarehe 13 Februari mliyoomba kuna mtu mwingine alishaomba tayari, wakauliza huyu mliyempa aliandikiwa wapi akasema kwenye faili, wakawaambia leteni hilo faili ili tumjue huyo mtu tuzungumze naye anaweza akatuachia hawakuletewe.”

Kigaila amesema baada ya kupewa maelezo hayo, Chadema iliamua kusogeza mbele tarehe ya maandamano jijini humo.

“Sababu ya kubadilisha tarehe ya maandamano ni hiyo ya kwamba tulikwenda tarehe 5 Februari tukaambiwa uwanja uko wazi tarehe 16 ikabadilika tukaamua tuchukue tarehe 15 badala ya tarehe 13,” amesema Kigaila.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Mwinyi aungana na Samia kuuaga mwili wa baba yake

Spread the loveRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk....

Habari za SiasaTangulizi

Mtoto wa Mzee Mwinyi amwaga machozi

Spread the loveMtoto wa Hayati mzee Mwinyi, Abdullah Ali Hassan Mwinyi ameshindwa...

Habari za SiasaTangulizi

Mzee mwinyi alikuwa mwanademokrasia wa kweli

Spread the loveMtoto wa Hayati Ali Hassan Mwinyi, Abdullah Ali Hassan Mwinyi...

Habari za SiasaTangulizi

Samia: Mwinyi alikuwa maktaba inayotembea

Spread the loveRais Samia Suluhu hassan amesema Hayati rais mstaafu, Ali Hassan...

error: Content is protected !!