Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema waanza kupanga mikakati ya kushughulikiana
Habari za SiasaTangulizi

Chadema waanza kupanga mikakati ya kushughulikiana

Antony Komu, Mbunge wa Moshi Vijijini (Chadema) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), kushoto ni Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea
Spread the love
UHASAMA na siasa za makundi vimeanza kushika kasi ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kufuatia baadhi ya viongozi wandamizi wa chama hicho, kuwandalia wabunge wao wawili audio inayolenga kuaminisha umma kuwa kunapanga njama zinasukwa dhidi ya Mwenyekiti anayemaliza muda wake, Freeman Mbowe. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Wabunge walioandaliwa audio hiyo, ni Anthony Komu (Moshi Vijijini) na Saed Kubenea (Ubungo). Wote wawili wamekana kilichomo kwenye video hiyo.

Akizungumzia na waandishi wa habari, leo tarehe 23 Novemba 2019, jijini Dar es Salaam, Komu amesema lengo la audio hiyo, ina lenga kuwadhoofisha wanachama wanaojitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama hicho.

Amesema, “…naomba watu waipuuze hasa wanachama wa Chadema, kwa sababu kuna picha inataka kujengwa na watu wanaotaka waonekane wao ni mashujaa na wengine ni wasaliti. Wanataka kukidhoofisha chama.” 

Amesema, “huu ni uongo. Ni muhimu ukapuuzwa. Vinginevyo, watu waje hadharani, waseme mimi fulani bin fulani, tulizungumza na fulani mahala fulani masuala ya kutengeneza uhaini au usaliti ndani ya chama. Siyo haya mambo ya kuchomeka.”

Kuibuka kwa wabunge hao kumekuja kufuatia sauti yenye mazungumzo, yanayodaiwa kuwa ni ya kwao na Joseph Selasini, mbunge wa Rombo (Chadema), wakijadili namna ya kuwang’oa viongozi wa chama hicho, kusambaa mitandaoni.

Akikazia hoja yake, Komu amesema, wala siyo kosa kwa mwanachama wa Chadema kuonesha nia ya kugombea uongozi wa chama hicho; na au kumuunga mkono mtu fulani.

“Kuna watu wanatajwa kwamba hao na wao wataingia kwenye kinyang’anyiro cha uenyekiti, mimi nafikiri kama kuna watu watachukua msimamo wa rafiki yangu Cecil Mwambe, wafanye hivyo. Yaliyofanywa na Mwambe ni jambo la kupongezwa.

“Sioni kama ni dhambi Mwambe kugombea na kama wako wengine wanaotaka kugombea. Hao wanaoweka hiyo picha kwamba wanaojitokeza kugombea ni uhaini au usaliti, ni kosa kubwa,” ameeleza Komu.

Komu amewashauri wanachama wa Chadema wenye nia ya kugombea nafasi mbalimbali wajitokeze, kwa kuwa ni haki yao.

Amese,a, “nawashawishi waje hadharani, wagombee ili atakaeshinda ionekane amefanya kazi. Ikiwa hivyo itakuwa afya. Kuliko hao wanaofikiri kama huo uchaguzi wa maigizo kama ulivyo wa serikali za mitaa, sisi kama chama cha upinzani kinachoongoza, tusiingie kwenye namna hiyo.” 

Kwa upande wake Kubenea, amesema kilichomo kwenye audio hiyo, ni vitu vilivyotengenezwa na kuungwa ungwa na hivyo, anaiomba Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), ifuatilie mazungumzo hayo, ili pamoja na mengine, kuwafahamu wahusika na kuwachukulia hatua.

“Sauti inayotembea imehaririwa. Nichukue nafasi hii kuiomba TCRA ifuatilie, ione nani aliyehusika kufanya kazi hiyo chafu. Mimi binafsi nitaandika barua TCRA ifuatilie kujua nani aliihariri,” ameeleza.

Kubenea amesema, kitendo cha sauti hiyo kuhaririwa na kusambazwa mitandaoni, ni muendelezo wa kampeni za makundi ya watu, wanaowapinga wanachama wanaoonesha nia ya kugombea kwenye uchaguzi wa viongozi wa Chadema.

Amesema, “Chama chetu ni cha demokrasia na tunatarajia huu uchaguzi watu watajitokeza, wagombee ili kuwe na ushindani.  Watu wasifanye wanaojitokeza kugombea ni uhaini. Siyo kweli. Nadhani hii audio imetengenezwa mahususi kwa ajili ya kumdhoofisha Selasini anayegombea uongozi Kanda ya Kaskazini. Huyu anachuana na Lema (Godbless Lema, mbunge wa Arusha Mjini),  ambaye amejipambanua kama kijana wa Mbowe.

“Niseme tuko kwenye uchaguzi na kila mtu yuko na mtu anayemuunga mkono.  Lakini anayeshinda anaungwa mkono. Tukishamaliza uchaguzi tunavunja makundi, na watu wote tunakuwa kitu kimoja. Na ndivyo inavyokuwa kwenye uchaguzi wote.” 

Wabunge hao wanadaiwa kupanga mipango ya kumhujumu Mbowe, Lema na mbunge wa Iringa Mjini na mwenyekiti wa Chadema, Kanda ya Nyasa, Peter Msigwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!