April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

JPM: Tumebembelezana sana, sasa basi

Rais John Magufuli

Spread the love

RAIS John Magufuli, amezipa siku 60 taasisi, mashirika na kampuni 187 za umma, ziwasilishe gawio serikalini. Anaripoti Hamis Mguta…(endelea).

Ametoa agizo hilo leo tarehe 24 Novemba 2019, Ikulu Ndogo, Chamwino mkoani Dodoma akipokea gawio kutoka taasisi, mashirika na kampuni 79 kati ya 266 za umma.

Aidha, amemuagiza Waziri wa Fedha, Dk. Philip Mpango kuchukulia hatua taasisi hizo, na kwamba isizidi miezi miwili kabla ya kuwasilisha gawio vinginevyo zijiondoe zenyewe.

“Tumebembelezana sana, hatuwezi kuendelea kukaa na mashirika, bodi na viongozi wa namna hii, fedha inaendelea kuteketea. Wasipokabidhi, bodi zijivunje zenyewe.

“Wapo wanaolipwa mishahara hadi milioni 15 kwa mwezi, halafu hakuna gawio, why (kwanini)?, haifai kuwepo, kwa hiyo Waziri Mpango nenda kapange hivyo na orodha yao ninayo, waziri uliniletea, kwahiyo umewachongoea,” amesema.

Amesema, ni vyema ukaanza mchakato wa kutengeneza mikataba na hata kama sheria ikipitishwa bungeni ya kuwa, mtu akipewa shirika na serikali ina shea, ukishindwa ikiwezekana ufungwe.

“Iwe hata serikali ina shea ya asilimia 5 ,lazima ulipe na mimi nafikiri tuanze kutengeneza mikataba hata ifike bungeni, kwamba ukipewa shirika na serikali inashea, usipolipa ufungwe.

“…na saa nyingine pawepo na uthubutu wa kwamba utazalisha usipozalisha hautakiwi kuwa hapo kwasababu umewacheleweshea watanzania wengi maendeleo yao,” amesema.

Katika wasilisho la gawio hilo, Waziri Mpango amesema, mapato ya makusanyo ya 2018/19 yanajumuisha mapato yaliyokusanywa kupitia akaunti chini ya msajili wa hazina.

Na kwamba, zilileta bilioni 683.23, fedha zilizopelekwa moja kwa moja mfuko mkuu wa serikali kutoka taasisi na mawakala wa usimamizi wa bandari (TPA), Mamlaka ya Viwanja vya ndege (TAA), Shirika la Maendeleo ya petroli (TPDC) na Bodi ya Michezi ya kubahatisha yalifikia bilioni 370.59.

Amesema, katika kipindi cha mwaka 2018/19 makusanyo ya mapato yanayopita katika akaunti ya msajili wa hazina yamevuka lengo kwa kukusanya bilioni 683.23 ikilinganishwa na malengo ya bilioni 597.77 ambayo ni asilimia 114.3 ya lengo.

Aidha, amesema mafanikio hayo yanatokana na sera na usimamizi bora wa mali za serikali ikijumuisha kuongezeka kwa mashirika yanayotoa gawio na michango pamoja na kuimarisha ufuatiliaji.

error: Content is protected !!