Tuesday , 19 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema kuja kivingine kesi ya Mbowe, wenzake
Habari za SiasaTangulizi

Chadema kuja kivingine kesi ya Mbowe, wenzake

Spread the love

 

CHAMA kikuu cha upinzania nchini Tanzania cha Chadema, kimesema hakijaridhishwa na uamuzi wa Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, dhidi ya uamuzi wa kesi ndogo ndani ya kesi kubwa inayomkabili kiongozi wa chama hicho, Freeman Mbowe na wenzake. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mapingamizi hayo yalihusu maelezo ya onyo ya mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo Adam Kasekwa, yasitumike mahakamani hapo kama sehemu ya ushahidi wa jamhuri na maelezo hayo yalitolewa baada ya Kasekwa kuteswa.

Katika uamuzi wake, Jaji Kiongozi Mustapha Siyani amesema, kulikuwa na sababu ya msingi ya kutolewa nje ya saa 4 kwa mujibu wa sheria na kuhusu kuteswa upande wa utetezi haujadhibitisha hilo.

Mara badaa ya uamuzi huo, uliotolewa asubuhi ya leo Jumatano, tarehe 20 Oktoba 2021, Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, amesema hawajaridhishwa na uamuzi uliotolewa na Kaji Kiongozi Siyani lakini sheria inawabana kukata rufaa dhidi ya uamuzi ulitolewa katika kesi ndogo, wakati kesi ya msingi ikiendelea kusikilizwa.

“Muhimu umma ukajua kama ambavyo hatukuridhika na maamuzi yaliyotoelewa awali katika kesi hiyo na Jaji Elinaza Luvanda, hatujaridhika na maamuzi yaliyotolewa leo Jaji Siyani.”

“Kama sheria ingeturuhusu kukata rufaa, mapema sana tungepanda mahakama ya juu kukata rufaa,” amesema Mnyika.

Mnyika amedai, hawajaridhika na uamuzi huo kwa kuwa Jaji Kiongozi Siyani hakuzingatia hoja za msingi za upande wa utetezi katika kesi hiyo ndogo, ikiwemo ya mtuhumiwa kiteswa wakati anachululiwa maelezo.

“Tutanzungumza kwa kina maeneo ambayo Jaji Siyani hajatenda haki, kwa uamuzi alioufanya mapingamizi mawili hakuzingatia hoja za msingi za utetezi,” amesema Mnyika.

Katibu Mkuu huyo wa Chadema amedai, maamuzi ya mahakama hiyo dhidi ya mapingamizi yaliyowasilishwa na upande wa utetezi katika kesi hiyo, yatatumika katika Mahakama ya Rufaa, kama hoja za uttezi endapo Mahakama hiyo ya Uhujumu uchumi itamkuta na hatia Mbowe.

Pingamizi la kwanza la Mbowe na wenzake, dhidi ya mamlaka ya mahakama hiyo kusikiliza mashtaka ya ugaidi, lilitupwa na Jaji Elinazer Luvanda, kabla hajajjitoa katika usikilizwa wa kesi ya msingi. Huku pingamizi la pili dhidi ya maelezo ya onyo ya mshtakiwa huyo, likitupwa na Jaji Siyani leo kabla ya kujitoa.

“Lakini uamuzi wa Jaji Luvanda na Siyani, zitakuwa hoja za msingi zitakazotumika baadae kama kutakuwa na njama za kumfunga mwenyekiti, zitatumika katika Mahakama ya Rufaa kama ilivyofanyika katika kesi ya Akwilina ambapo kwenye mahamama ya chini tulionekana wakosaji lakini mahakama ya juu iliamua sisi hatuna hatia,” amesema Mnyika.

Mnyika amesema, Chadema kitakutana kwa ajili ya kujadili uamuzi huo.
“Leo tukitoka hapa tunakwenda kukutana kama chama kutafakari kwa kina, wakati mawakili wakiongea na watuhumiwa. Uamuzi uliotolewa haukuzingatia haki, tutachambua maeneo ambayo jaji hakutenda haki,” amesema Mnyika

Mnyika amesema, Chadema kitatumia njia nyingine kutafuta uhuru wa Mbowe na wenzake.

“Tutaendelea na mapambano ya kutafuta haki kwenye mahakama hii, mapamabano yatendelea kwa jaji mwingine. Lakini tutatumia vilevile njia nyingine za kutafuta haki ili haki ipatikane kwa wakati,” amesema Mnyika na kuongeza:

“Siku 92 za kukaa ndani na maeleozo ya jaji anaonesha kesi itachukua meizi mingine mwili au mitatu, maana yake tunaingia kwenye kundi la haki kucheleweshwa. Kwa vyovyote vile lazima kila mpenda haki tuungane pamoja kudai haki ipatikane mapema.”

Akitoa uamuzi katika pingamizi la muda, Jaji Kiongozi Siyani amesema, kifungu namba 50 (2) na cha 51 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, iliyofanyiwa marekebisho 2019, kinaruhusu muda wa kumhoji mtuhumiwa kuongezwa kwa masharti maalum, ikiwemo mkuu wa upelelezi kuongeza muda kwa ajili ya kufanya upelelezi au kuomba kibali cha kuongeza muda huo mahakamani.

Jaji Kiongozi Siyani amesema, hoja ya jamhuri kuchelewa kumhoji Kasekwa kwa sababu ya mtuhumiwa huyo kuwasaidia kumtafuta mwenzao, Moses Lijenge mkoani Kilimanjaro na Arusha na kumsafirisha kutoka Moshi kuja Dar es Salaam, ina mantiki.

Mbali na Mbowe na Kasekwa, watuhumiwa wengine katika kesi ya msingi ya uhujumi uchumi yenye mashtaka ya kula njama za kufanya vitendo vya ugaidi ni, Halfan Hassan Bwire na Mohammed Abdillah Ling’wenya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Zanzibar mbioni kuanza uchimbaji mafuta na gesi baharini

Spread the loveSERIKALI ya Zanzibar, imekamilisha mchakato wa uchimbaji wa mafuta na...

Habari za Siasa

Wizara ya afya yataja mafanikio 10 miaka mitatu Samia madarakani

Spread the loveWIZARA ya Afya imetaja mafanikio 10 iliyoyapata ndani ya miaka...

Habari za Siasa

Mbozi walilia kuwa manispaa, majimbo 3

Spread the loveHALMASHAURI ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe imeeleza dhamira yake...

Habari za Siasa

Wabunge waitaka TPDC kuongeza kasi ya kuunganisha wateja gesi asilia

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini...

error: Content is protected !!