Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CCM ya Dk. Nchimbi yaanika mikakati ya kuwaangamiza wapinzani
Habari za Siasa

CCM ya Dk. Nchimbi yaanika mikakati ya kuwaangamiza wapinzani

Dk. Emmanuel Nchimbi
Spread the love

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimetangaza mikakati ya kupata ushindi katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2024 na Uchaguzi Mkuu wa mwakani, huku kikituma salamu kwa wapinzani kwamba lazima kitimize lengo la kuendelea kushika dola. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Mikakati hiyo imetajwa leo tarehe 5 Aprili 2024 na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Amos Makalla, katika hafla ya ukaribisho wa wajumbe wapya wa Sekretarieti ya chama hicho, walioteuliwa hivi karibuni.

Wajumbe hao ni, John Mongella, aliyeteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara. Jokate Mwegelo (Katibu Mkuu UVCCM) na Ally Salum Hapi (Katibu Mkuu Jumuiya ya Wazazi).

Makalla amesema wajumbe hao kwa kushirikiana na Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Emmanuel Nchimbi, watahakikisha mikakati hiyo inatekelezwa kikamilifu kwa ajili ya kupata ushindi.

“Tunaye katibu mkuu Dk. Nchimbi, tunaye naibu katibu mkuu mpya na mimi nikaongezewa, nataka niwahakikishie timu imekamilika na uzuri sekretarieti hii tunajuana boss wetu tunamheshimu kwa sababu yeye ametuongoza, ametutengeneza, nataka kuwahakikishia tutafanya kazi kubwa iliyokusudiwa na chama chetu kuhakikisha kinapata ushindi mkubwa,” amesema Makalla.

Makakati wa kwanza alioutaja Makalla ni kuwafikia viongozi wa CCM wa ngazi za chini na wananchi wa kawaida, ili kuwaandaa kwa ajili ya ushindi wa chaguzi zijazo.

“Nataka niwahakikishie kazi yetu kwa sasa tukiongozwa na katibu mkuu tunarudi kwa wanachama wetu na wananchi wa kawaida, hayo ndio maandalizi tutalala huko, tutapiga kambi lazima kieleweke. Msingi wa chama chetu unaanzia chini kwa mabalozi na wajumbe wa mashina na matawi kuwaandaa kwa ajili ya ushindi wa uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa mwakani,” amesema Makalla.

Makalla amesema “uchaguzi ni kura, uchaguzi ni namba bila ya kuwa wapiga kura walioandaliwa hauwezi kushinda, ndio maana tunataka kuja huko tushinde kwa kishindo.”

Makalla ametaja mkakati mwingine kuwa ni kutangaza kazi zilizofanywa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, katika kuwafikishia huduma za kijamii wananchi wa chini, kama huduma ya maji, barabara, umeme na maji.

“Mkakati mwingine uliotajwa na Makalla, ni wa chama hicho kuwa katibu na makundi ya wananchi wa chini kama wajasiriamali, madereva wa bodaboda na mamalishe.

“Ushauri wangu makundi yote haya tuendelee kuyakumbatia, tufanye nayo kazi tutapata ushindi. Ningeshauri serikali muyakumbatie makundi haya ya wamachinga, bodaboda, mama lishe ili CCM ibaki kuwa kimbilio la wananchi. Tuwasilikilize wananchi,” amesema Makalla.

Aidha, Makalla amesema watahakikisha wanatekeleza falsafa za maridhiano zilizoasisiwa na Rais Samia, ikiwa pamoja na kufanya siasa za kistaarabu na kujibu hoja kwa hoja badala ya vihoja.

“Nataka niwakumbushe wote, harakati za vyama vyovyote vya siasa ni kushika dola na kama lengo ni kushika dola maana yake kuunda serikali ya CCM, nataka niseme kama hilo ndilo lengo la chama cha siuasa kushika dola maana yake ni kuanza kushinda uchaguzi wa serikali za mitaa na ukitaka kushinda vizuri uchaguzi mkuu lazima upate ushindi mkubwa kwenye serikali za mitaa, hilo halina mashaka kwa safu hii,” amesema Makalla.

Naye Naibu Katibu Mkuu CCM Bara, John Mongella, amesema kazi ndio imeanza kwa chama chake kusaka ushindi wa chaguzi zijazo.

“Mmemsikia Makalla, maana yake mziki umeanza na mimi nataka kusema kama kuna mtu alikuwa hamuelewi vizuri Rais Samia, hii safu ni ujumbe tosha,” amesema Mongella na kuongeza:

“CCM ina kazi ya kutafuta dola, kwa hiyo katika kushika dola hakuna kubembelezana, tukimaliza kushika dola serikali za mitaa na uchaguzi mkuu tutakuja mezani kunywa kahawa na jambo hili wala halina mzaha.

1 Comment

  • Upinzan hauwezmalizwa na maneno ya team hiyo Kwa kutumia dola, utekaj, kuiba kura, nk. Mkakati muhimu ulitakiwa kumaliza ufisadi na ubadhilifu wa fedha za umma. Wote hao wanajulikana Kwa wizi na sisi tutaanika kote Hadi vijijin waskojulikana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!