Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CCM: Hatutawabeba viongozi mizigo chaguzi zijazo
Habari za Siasa

CCM: Hatutawabeba viongozi mizigo chaguzi zijazo

Daniel Chongolo, Katibu Mkuu wa CCM akizungumza na wajumbe wa chama hicho
Spread the love

 

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema hakitawabeba viongozi mizigo katika chaguzi zijazo, huku kikiwataka waliopewa dhamana wakati huu kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi ili kujenga imani kwa wananchi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Rukwa … (endelea).

Onyo hilo limetolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Idara ya Oganaizesheni, Issa Ussi Gavu, akizungumza na wananchi pamoja na viongozi wa chama hicho Wilaya ya Nkasi, mkoani Rukwa.

“Niwaombe sana wetu nendeni mkatimize wajibu wenu na sisi kama CCM hatutakuwa tayari kumbeba, kumsaidia au kuhakikisha kwamba mtu asiyetimiza wajibu wake sisi tunamtia kwenye mbeleko. Umbeleko wa CCM utambeba kiongozi aliye tayari kujitoa, kutenda na kuwatumikia anaowaongoza,” amesema Gavu.

Gavu amewataka wenyeviti wa vitongoji, vijiji na mitaa wakatekeleze majukumu yao kwa mujibu wa sheria, huku akiwasisitiza kutoa taarifa za mapato na matumizi kwa wananchi wao ili kuwaondoa mashaka juu ya matumizi ya mapato.

“Mnatakiwa muitishe vikao vya mapato na matumizi kwenye maeneo yenu ili wananchi wapate taarifa zilizo sahihi, kilichopatikana, kilichotumika, faida na kasoro zake ili kupunguza mashakama kwa jamii unayoiongoza na kujenga imani na upendo kwako pamoja na chama na serikali,” amesema Gavu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!