Wednesday , 1 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Bunge la Tanzania lashauri corona igeuzwe fursa
Habari za Siasa

Bunge la Tanzania lashauri corona igeuzwe fursa

Spread the love

KAMATI ya Kudumu ya  Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji nchini Tanzania, imependekeza wakati huu dunia ikiwa kwenye janga la ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababishwa na virusi vya corona (COVID-19) nchi ijikite kwenye kilimo cha umwagiliaji ili inufaika kwa kuuza chakula nje. Anaripoti Faki Sosi …(endelea).

Akiwasilisha mapendekezo hayo Mahmoud Mgimwa-Mwenyekiti wa Kamati hiyo leo Jumanne tarehe 12 bungeni jijini Dodoma amesema, ugonjwa wa COVID-19 unaweza kuwa fursa kwa mazao ya kilimo.

Amesema wakati huu nchi ikizalisha chakula cha kutosha nchi itanufaika kwa kuuza chaula nje ya nchi.

“Pamoja na kuwepo viashiria vya mdororo wa sekta mbalimbali ikiwepo sekta ya kilimo, kamati inaamini changamoto hiyo ni fursa kwa nchi yetu kutokana na kuwa na uwezo wa kuzalisha chakula cha ziada na hata kuweza kuuza nje ya nchi hususan kipindi hiki cha janga la COVID – 19,” amesema Mgimwa.

Amesema, Tanzania inarutuba na ardhi ya kutosha hivyo Serikali ikiwekeza kwenye kilimo cha umwagiliaji itanufaika.

Wakati huo huo, kamati hiyo imeishauri serikali kutoa ruzuku kwa wakulima kwa ugonjwa wa COVID-19 umeathiri kilimo.

“Ili kukabiliana na janga la (COVID-19) na kupelekea shughuli za kilimo kuathirika kwa kiasi kikubwa zinapaswa kusaidiwa kwa Serikali kutoa ruzuku kwa wakulima, kuangalia uwezekano wa kupunguza au kuondoa riba za mikopo kupitia taasisi za fedha na au kuongeza muda wa kulipa mikopo iliyokwisha tolewa ili kuwezesha wakulima na kilimo kuendelea kuzalisha,” amesema.

Kamati hiyo imeitaka Serikali kutenga asilimia kumi la pato la taifa ili kuendeleza sekta ya kilimo katika kuviwezesha kifedha vituo vya utafiti ili wataalamu wa utafiti waweze kufanya tafiti zenye manufaa kwa nchi.

Imeshauri kwenye asilimia hiyo ya pato la taifa serikali iwezesha kifedha Wakala wa Taifa wa Uzalishaji na uendelezaji wa mbegu za kilimo (ASA) ili kuhakikisha nchi inakuwa na usalama wa chakula unaotokana na matumizi sahihi ya mbegu bora ambazo zitapatikana kwa urahisi na kuwafikia wakulima kwa wakati na kwa gharama nafuu.

Kamati hiyo imesisitiza umuhimu wa kuiwezesha kifedha Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ili kuweza kutekeleza miradi ya kimkati itakayosaidia kuwa na uhakika wa kilimo katika msimu wa mwaka mzima bila kutegemea kilimo cha mvua ambacho sio cha uhakika kwa sasa kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Wakati huo huo, kamati hiyo imeitaka serikali kuacha kuwatoza ushuru watengeneza mbolea wa ndani ili kuweka mizania ya usawa kwa kuwa wanaoingiza mbolea kutoka nje hawatozwi.

Katika kumlinda mtengeneza mbolewa wa ndani kamati imeishauri serikali kabla ya kutoa vibali ya kuagiza mbole nje ya nchi, ni vyema tathimini ikafanyika ili kufahamu mbolea inayozalishwa nchini na pungufu ndio iagizwe.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!