Spread the love

 

MWENYEKITI wa Baraza la Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Mhandisi Richard Masika ameruhusu wakufunzi waliofikia umri wa kustaafu kuendelea kufanya kazi ili kurithisha ujuzi kwa vijana. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

“Wapo wakufunzi ambao wamefikia umri wa kustaafu, sisi bado tunaruhusu waendelee kufanya kazi ili kutumia ujuzi wao walioukusanya na kuwafunza hawa wadogo waliopingia ili kuyajenga makampuni yao,” amesema

Mhandisi Masika amesema hayo leo Alhamisi, tarehe 30 Desemba 2021, katika wakati akizindua bodi ya taasisi hiyo kitengo cha ushauri wa kitaalamu (DIT-ICB). Pia, alikagua shughuli mbalimbali za kitaalamu zinazofanywa na kitengo hicho.

Amesema, kitengo hicho kimeanza kipindi, “muhimili wa maendeleo katika taifa letu ni ufundi na teknolojia na kwa sasa DIT inatambulika na kuheshimika kwa mchango wake mkubwa nchini Tanzania.”

“Maonesho haya yameonesha tuna uwezo gani upande wa vifaa vinavyoweza kutumika kutoa ushauri wa kitaalamu na tumeona tuna wabobezi waliopo hapa DIT wanavyoweza kutumika ikiwemo eneo la madini, tafiti aina ya miamba na uchimbaji pamoja na upasuaji wa miamba,” amesema Mhandisi Masika.

Aidha, Mhandisi Masika amesema, “tumeona majengo mengi yaliyojenga eneo la Tanzania upimaji wake unaweza kufanywa nchini na majengo yanayojengwa baharini yanaweza kupimwa huko miamba ya aina gani.”

“Watanzania wamini kwamba tunao vijana wanaoweza kufanya kazi nyingi sana za utoaji wa kitaalamu na hizi kazi zinafanywa na wakufunzi na walimu wao ili kuwajengea uwezo ili siku moja waweze kuanzisha kampuni zao zitakazoendelea kufanya kazi hizo,” amesema

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya DIT-ICB, Profesa Patrick Nsimama, amesema ili kitengo hicho kiwezi kusonga mbele lazima kiwe na bodi na “mimi nikiwa mwenyekiti nitasimama vizuri na kutumika ili mafanikio na huduma mbalimbali tunazozitoa za uhandisi na teknolijia ziwe za kiwango kikubwa zaidi na kugusa miradi ya kimkakati.”

Profesa Nsimama ambaye pia ni Naibu Mkuu wa DIT-Taalamu, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu amesema, “maelekezo yaliyotolewa ni mazuri na ya msingi na sisi tutakwenda kuyafanyia kazi ili tuweze kusonga mbele.”

Naye Mhandishi Johnson Malisa, Meneja wa ICB alisema, tangu kuanza kwa kitengo hicho, wamefanyikiwa kushiriki katika kazi mbalimbali ikiwemo usanifu wa awali wa mradi reli ya kisasa (SGR), kusimamia ubora wa vifaa vinavyotumika kwenye ujenzi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere.

“Tunahakikisha thamani ya fedha inapatikana na kitengo hiki kimeaminiwa na serikali na kukitumia kitengo chetu katika kazi mbalimbali kwa kushiriki kwenye miradi,” amesema Mhandisi Malisa

Amesema, kitengo hiki ni cha kipekee kwani kinashirikiana kati ya walimu na wanafunzi.

“Mwanafunzi anakuwa na nafasi ya kujifunza kutoka kwa walimu na kupata uelewa wa kutosha na kwenda kutumika kwenye ujenzi bila kupitia sehemu nyingine za nje ya nchi,” alisema Mhandisi Malisa

Ameongeza, “miradi yetu imekuwa kielelezo kwa walimu na wanafunzi na wengine wanabaki hapa kuendelea na wengine wanakwenda maeneo mbalimbali kama Tanroads na bodi hii itasimamia vyema kitengo hiki ili kiwe bora zaidi..”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *