November 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ajibu avunja mkataba na simba, aibukia Azam FC

Spread the love

 

KIUNGO mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Simba Ibrahim Ajibu amejiunga rasmi na matajiri wa jiji la Dar es Salaam, klabu ya Azam FC mara baada ya kuvunja mkataba wake na klabu yake ya zamani kwa makubaliano ya pande zote mbili. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Ajibu ameondoka ndani ya klabu ya Simba mara baada ya kuhudumu kwa miaka nane katika vipindi tofauti, toka alipopandishwa kutoka timu ya viajana ya Simba mwaka 2013 akiwa na umri wa miaka 17.

Leo tarehe 30 Desemba, 2021 klabu ya Azam FC ilimtambulisha rasmi mchezaji huyo ambaye amekwenda kuchukua nafasi ya Salum Abukar “Sure Boy” ambaye ametimka Yanga.

Kwenye utambulisho wake Ajibu hii leo amekabidhiwa jezi namba nane tayari kawa ajili ya kuwatumikia matajiri hao wa jiji.

Usajili huo wa Azam Fc unamfanya Ajibu kuwa kati ya wachezaji wachache waliofanikiwa kucheza klabu zote kubwa nchini Simba, Yanga na Azam FC.

Muda machache mara baada ya kutambulishwa Azam Fc, klabu ya Simba ilitoa taarifa rasmi ya kuachana na mchezaji kwa makubaliano binafsi kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii na kumtakiwa kila la kheri.

error: Content is protected !!