Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Bodi 100 taasisi za kisiasa, dini njiapanda 
Habari za Siasa

Bodi 100 taasisi za kisiasa, dini njiapanda 

Spread the love

WAKALA wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) nchini Tanzania, imezitaka Bodi za Wadhamini wa Taasisi 100 ambazo hazijafanya marejesho ya wadhamini kufanya hivyo haraka kabla hatua hazijachukuliwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea)

Taasisi hizo ambazo hadi kufikia Juni 2020 zilikuwa hazijawasilisha marejesho zipo taasisi za dini, kisiasa na kijamii.

Miongoni mwa vyama hivyo vya siasa ni TLP, NRA, DP, Tadea, UPDP, UDP na UMD.

Taarifa iliyotolewa jana Jumatano tarehe 2 Septemba 2020 na Emmy Hudson, Msimamizi Mkuu wa Wadhamini wa Rita imesema, wakala wanaendelea na shughuli ya uhakiki wa kina wa Bodi za taasisi zote zilizosajiliwa chini ya Sheria ya Usajili wa Wadhamini  Sura ya 318,lengoili kufahamu hali ya kila taasisi kama zinatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria na katiba za taasisi husika.

“Wakati uhakiki ukiendelea, Bodi za taasisi hizo zinatakiwa kuwasiliana na Wakala ili kuhakiki taarifa zao na kwa upande wetu Rita tayari tumeanza kuzitembelea ofisi za taasisi hizo,” amesema Emmy.

Taarifa hiyo imesema, nuunganisho wa wadhamini ni utaratibu unaohusisha usajili wa wadhamini ambao huwezesha wadhamini waliounganishwa kuwa na utu wa kisheria, kuweza kushitaki au kushitakiwa kwa jina lake, kumiliki na kuuza mali na kuingia katika mikataba kwa niaba ya taasisi hizo.

“Kwa mujibu wa Sheria, Bodi ambazo hazitekelezi majukumu yake kikamilifu zinatakiwa kufutwa katika Daftari la Msimamizi Mkuu wa Wadhamini na zitapaswa kurejesha mara moja hati za usajili kwa Kabidhi Wasii Mkuu kulingana na kifungu cha 23(4) cha Sheria ya Usajili wa   Wadhamini.”

“Mali za Taasisi/Asasi hizo zinawezwa kuwekwa chini ya usimamizi wa Mdhamini wa Umma (Ofisi ya RITA) endapo kutakuwa na ombwe la Wadhamini mpaka hapo utaratibu mwingine utakapotolewa,” imeeleza taarifa hiyo

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

error: Content is protected !!