March 3, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Bobi Wine alazwa ICU, madaktari wasema alipewa sumu

Spread the love

MBUNGE wa Kyadondo Mashariki nchini Uganda, Robert Kyagulanyi hali yake kiafya ni tete, amelazwa katika chumba cha uangalizi maalumu (ICU) nchini Marekani alikokwenda kupatiwa matibabu. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Taarifa kutoka kwa madaktari wanaomuuguza Kyagulanyi ambaye kwa jina maarufu anafahamika kama ‘Bobi Wine’, zianeleza kuwa mwanasiasa huyo yuko katika uangalizi maalumu kutokana na ogani zake za ndani kuharibika.

Kuharibika kwa ogani za ndani za Bobi Wine  kumemsababishia  mwanasiasa huyo kupata tatizo la damu kuvuja ndani kwa ndani, na kwenye matundu ya pua na masikio.

Vile vile, taarifa hiyo inaeleza kuwa, Bobi Wine alipokuwa kizuizini alichomwa sindano yenye sumu.

Bobi Wine amepata matatizo ya kiafya baada ya kuwekwa kizuini hivi karibuni, ambapo inadaiwa aliteswa na kupigwa na maafisa wa usalama.

error: Content is protected !!