
Spread the love
RAIS John Magufuli amemteua Kamishna wa Polisi, Diwani Athuman kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU). Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).
Taarifa ya uteuzi huo imetolewa leo tarehe 6 Septemba, 2018 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa.
Kamishna Diwani anachukua nafasi ya Kamishna wa Polisi, Valentino Mlowola aliyeteuliwa kuwa Balozi.
“Uteuzi wa Kamishna Diwani Athumani unaanza leo tarehe 6 Septemba 2018,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.
Kabla ya uteuzi huo, Kamishna Diwani alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera.
More Stories
Uchaguzi wa wanawake Chadema waingiliwa
Dk. Mwinyi amteua Dk. Mkuya, Nassor Mazrui
Waziri Majaliwa aitaka TPA kuongeza umakini