Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ngono chap chap yapigiwa chapuo bungeni  
Habari za Siasa

Ngono chap chap yapigiwa chapuo bungeni  

Spread the love

 SUSAN Lyimo, Mbunge wa Viti Maalum Chadema ametaka kutengenezwa mazingira ili wanaotaka kufanya ngono haraka, wawe  na amani. Anaandika Mwandishi Maalum…(endelea).

Lyimo ameitaka serikali kuruhusu watu kujipima wenyewe maambukizi ya Virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Ukimwi (VVU) ili wanaotaka kufanya mapenzi haraka wafanye wakiwa na uhakika wako salama.

Akiuliza swali hilo bungeni jijini Dodoma leo Alhamisi Septemba 6, Lyimo alisema kwa sasa wananchi wana uelewa kuhusu masuala ya ugonjwa wa Ukimwi ambapo alitaka kujua ni kwa nini serikali hairuhusu watu kujipima wenyewe kwa kipimo cha haraka (Rapid HIV Test).

“Mwenyekiti ukienda Vituo vya Afya usiku vimefungwa na kuna watu wanataka kufanya ‘chap chap’ kwa nini wasiruhusiwe wafanye vipimo hivyo ili waende kwenye shughuli hiyo wakijua wako salama,” amehoji Lyimo.

Aijibu swali hilo, Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amesema kwa mujibu wa Sheria ya Afya, upimaji unafanyika Kituo cha Afya lakininpia serikali imeanza mchakato wa sheria hiyo ili watu waweze kujipima wenyewe.

“Lakini kumeibuka mjadala kuna wengine wanasema mtu akijipima mwenyewe ataendabkuambukiza wengine.

“Kwa hiyo kwanza tutaanza kuruhusu mtu ajipime mwenyewe lakini mbele ya Ofisa wa Afya katika Kituo cha Afya, hayo ndiyo mapendekezo tuliyotoa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na tutauleta bungeni ili wabunge mtusaidie,” amesema Mwalimu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

Habari za Siasa

CCM yakemea ufisadi, yaipa kibarua TAKUKURU

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimekemea vitendo vya ubadhirifu wa...

Habari za Siasa

Bajeti ya Ikulu 2024/25 kuongezeka, bunge laombwa kurudhia Sh. 1.1 trilioni

Spread the love  WIZARA ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa...

error: Content is protected !!