Wednesday , 8 May 2024
Home Kitengo Biashara Bilioni 650 kumaliza changamoto ya mbegu
BiasharaHabari Mchanganyiko

Bilioni 650 kumaliza changamoto ya mbegu

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe
Spread the love

WAZIRI wa Kilimo, Hussein Bashe amesema inahitajika uwekezaji wa shilingi bilioni 650, ili kumaliza changamoto ya upatikanaji wa mbegu bora na salama. Anaripoti Selemani Msuya …(endelea).

Bashe amesema hayo leo Ijumaa wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu wizara na Taasisi ya John Deere kutoa trekta kwa kikundi cha vijana ambacho kitaandika andiko zuri lenye kuweza kuleta mapinduzi kwenye kilimo.

Amesema kwa sasa Tanzania inazalisha mbegu tani 60,000 ambayo ni asilimia 50, huku hitaji likiwa tani 120,000, hivyo mikakati ya wizara ikifika 2025 wawe wamezalisha asilimia 75 ya hitaji.

“Kweli Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza wizara ishirikiane na taasisi zake ili ifikapo 2025, tuwe tumezalisha asilimia 75 ya mbegu na hili tutalifikia kwani kwa sasa tunazalisha asilimia 50 ya hitaji,” amesema.

Waziri Bashe amesema iwapo fedha hizo zitapatikana lengo la Tanzania kuzalisha mbegu zote hapa nchini litafikiwa, hali ambayo itawezesha kuondokana na uagizaji kutoka nje.
Amesema mikakati iliyopo ni kuanzisha mashamba ya mbegu na kuwapa wazalishaji katika sekta binafsi, hali ambayo itarahisisha zoezi hilo.

“Tunataka mbegu bora na salama na hili litafanikiwa pale ambapo kila mdau atashiriki, hivyo tunawakaribisha wadau wengine kuja kuwekeza katika eneo hili,” amesema.

Kuhusiana na kuandaa shindano la vikundi vya vijana kuwasilisha maandiko ya kushinda trekta, Waziri Bashe amesema lengo la wizara na serikali ni kuinua vijana wenye uhitaji wa kushiriki kilimo.

Bashe amesema muda ukifika watatangaza ili vikundi hivyo viweze kushiriki na ambaye atakuwa na andiko zuri atapewa zawadi ya trekta.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Expanse Tournament kasino mzigo umeongezwa hadi mil 400/=

Spread the love Jiunge na Meridianbet kasino kufurahia promosheni kubwaya Expanse Tournament,...

Biashara

Bounty Hunters sloti yenye utajiri Meridianbet kasino

Spread the love Congo DR inasifika sana kwa wingi wa madini ya...

Habari MchanganyikoMichezo

Kengold wakabidhiwa kombe NBC Championship

Spread the loveMdhamini mkuu wa Ligi Daraja la Kwanza (NBC Championship) Benki...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

error: Content is protected !!