Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Bihimba atoa msaada ujenzi wa madrasa
Habari Mchanganyiko

Bihimba atoa msaada ujenzi wa madrasa

Spread the love

MWANAHARAKATI huru, Bihimba Mpaya ametoa msaada wa mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa madrasa iliyopo katika msikiti wa Aisha, Kivule jijini Dar es Salaam. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Bihimba ametoa msaada huo jana tarehe 26 Januari 2024, baada ya swala ya Ijumaa iliyofanyika msikitini hapo, jijini Dar es Salaam.

“Namshukuru Mungu leo tumeswali pamoja katika msikiti huu uliopo eneo la Mgambo Mtaa wa Kivule. Nimetoa saruji mifuko 10 kwa ajili ya ujenzi wa madrasa. Tunafanya haya kwa niaba ya Allah ili kujenga nyumba za kumuabudia na hii si mara ya kwanza mara nyingi nimekuwa nikichangia ujenzi wa msikiti huu,” amesema Bihimba.

Naye kiongozi wa msikiti huo, Sheikh Ramadhan Ally alisema “ tunashukuru leo tumepokea mzigo huu wa simenti kutoka kwa muumini mwenzetu. Tunashukuru tuko pamoja naye na tuko tayari kushirikiana naye katika ujenzi huu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!