Sunday , 28 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Benki ya Exim yang’ara tuzo za mwajiri bora
Habari Mchanganyiko

Benki ya Exim yang’ara tuzo za mwajiri bora

Spread the love

BENKI ya Exim Tanzania imeendelea kutamba kwenye tuzo za mwajiri bora mwaka 2022 (EYA 2022) baada ya kuibuka kinara kwenye kipengele cha Mwajiri bora kutoka ndani ya nchi. Pia imeibuka mshindi kwenye kipengele cha usimamizi bora wa utendaji kazini. Anaripoti Mwandishi Wetuy … (endelea).

Tuzo hizo zimetolewa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Phillip Isdor Mpango.

Mkuu wa Idara wa Rasirimali watu wa benki ya Exim Tanzania, Frederick Kanga (Kulia) akipokea tuzo kutoka kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Prof. Joyce Ndalichako baada ya benki hiyo kuibuka kinara kwenye tuzo za Mwajiri Bora wa Mwaka 2022 (EYA 2022) kipengele cha Mwajiri bora kutoka ndani ya nchi zilizoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE). Hafla ya utoaji wa tuzo hizo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Prof. Joyce Ndalichako.

Awali akizungumza kwenye hafla ya tuzo hizo Dk. Mpango aliwahimiza waajiri wote kuboresha maslahi ya wafanyakazi kulingana na nafasi zao huku akibainisha kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha sera na sheria za nchi zinakidhi vigezo vya ajira na waajiriwa.

“Natambua pia juhudi za ATE katika kuhakikisha inasimamia vyema majukumu ya pande zote yaani baina ya mwajiri na mwajiriwa katika sehemu za kazi. Hatutaki malalamiko ya wafanyakazi yafike juu kabisa tunataka waajiri mtoe haki na stahiki za wafanyakazi wenu kwa mujibu wa miongozi iliyopo,” alisema.

Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hizo, Mkuu wa Idara wa Rasimali watu wa benki ya Exim, Frederick Kanga alisema mfululizo wa tuzo hizo kutoka ATE  ni kiashiria tosha mbele ya jamii kuhusiana na namna ambavyo benki hiyo imewekeza kwenye rasilimali watu, hatua ambayo ina umuhimu mkubwa katika kufanikisha malengo ya benki hiyo.

“Tuzo hizi kwetu ni mwendelezo wa sherehe zetu katika kuadhimisha miaka 25 tangu kuanzishwa kwa benki yetu. Katika maadhimisho hayo agenda ya rasilimali watu ilikuwa ni moja vya vipaumbele vyetu na leo hii tunakamilisha rasmi sherehe hizo kwa tuzo hizi muhimu zinazothibitisha dhamira yetu ya uwekezaji kwa wafanyakazi wetu,’’ alisema Kanga.


Mkuu wa Idara wa Rasimali watu wa benki ya Exim Tanzania, Frederick Kanga (wa tatu kushoto) pamoja na wafanyakazi wengine wa benki hiyo wakifurahia baada ya kutwaa tuzo za Mwajiri Bora wa Mwaka 2022 (EYA 2022) kipengele cha Mwajiri bora kutoka ndani ya nchi na kipengele cha usimamizi bora wa utendaji kazini zilizoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE). Hafla ya utoaji wa tuzo hizo iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

 

Alibainisha kuwa moja ya vipaumbele vya benki hiyo ni pamoja na kuwaandaa watendaji wake kwa kuwaongezea ujuzi unaowawezesha kuwa mbele ya wakati katika utendaji wao ili kuleta matokeo bora na yenye ubunifu mpya kwa wateja.

“Lengo ni kuifanya taasisi yetu iwe sehemu ambayo mfanyakazi anakuwa bora zaidi, mwenye mabadiliko na mwenye utofauti,’’ alisisitiza.

Kwa mujibu wa Kanga benki hiyo imedhamiria kuandaa wafanyakazi wenye ushirikiano katika kuunda timu imara ya pamoja kwa kuandaa mazingira ambayo wafanyakazi hao watajihisi kuwa wanathaminiwa, wanashirikishwa sambamba na kupewa fursa ya kukua na kujiendeleza kitaaluma.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mvungi aendesha kikao kazi cha wataalam wa Regrow

Spread the love  MKURUGENZI wa Idara Sera na Mipango Wizara ya Maliasili...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

Polisi wakanusha kufanya uzembe ajali iliyouwa mwandishi Ayo Tv

Spread the loveJESHI la Polisi limekanusha tuhuma zilizoibuliwa dhidi yake  kwamba limekawia...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia kuzindua gazeti litakalotoa habari za wafanyakazi Tanzania

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), liko mbioni kufufua...

error: Content is protected !!