Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Waliobomelewa nyumba Morogoro wamuangukia Samia, wamtaja Magufuli
Habari Mchanganyiko

Waliobomelewa nyumba Morogoro wamuangukia Samia, wamtaja Magufuli

Spread the love

WAKAZI wa Mtaa wa CCT mkoani Morogoro wameangua vilio baada ya serikali wilayani Mvomero kutumia jeshi la polisi, magereza pamoja na jeshi la akiba (mgambo) kubomoa nyumba zaidi ya 500 kwa kile kinachodaiwa kuwa wananchi hao wamevamia hifadhi ya msitu wa kuni. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)

Vilio vya wananchi hawa vilisikika mwishoni kwa wiki baada ya nyumba zao kuanza kubomolewa muda wa saa 11 alfajiri huku baadhi ya wananchi wakiwa bado hawajamka.

Mariam Hamis ni miongoni mwa wananchi waliokumbwa na kadhia hiyo ambapo pamoja na mengine alisema ameuza mabeseni ya machungwa maeneo ya Masika na fedha alizozipata alinunua kiwanja na kujenga nyumba yenye vyumba viwili ila anashangaa kuona nyumba yake imebomolewa.

“Baada ya kukosa kodi niliamua kuhamia kwenye kiwanja changu nikitumia mashuka kujistiri na baada ya kupata fedha nilijenga nyumba ya vyumba viwili… leo hii nyumba yangu inabobolewa jamani Mama Samia tuonee huruma”alissema Mariam.

Mama huyo alisema kuwa wakazi wa eneo hilo wameanza kuishi wakati wa utawala wa Rais wa John Magufuli na hapakuwa na tatizo lolote lakini kwa sasa wanaokekana kuwa wao ni wavamizi ambapo alihoji kuwa huo uvamizi mbona hapo awali haukuwepo.

Mariam alimuomba Rais Samia Suluhu Hassan kusikia kilio cha wananchi wakazi wa eneo hilo na kuwasaidia kwani kitendo cha kubomoa nyumba zao kimewafanya wakose makazi na hawajui hatima ya maisha yao yatakuaje katika kipindi hiki.

Kwa upande wake Juma Manyanda alisema amesikitishwa na kitendo hicho cha kinyama kwani wakati wananchi hususan yeye anakwenda kununua kiwanja eneo hilo alielekezwa mpaka na kwamba vielelezo vinampa kibali cha kujenga.

Manyanda alisema kuwa watu wamekuwa wakijenga nyumba zaidi ya miaka mitatu iliyopita na hakuwahi kuona katazo la kuzua watu wasijenge nyumba ila anashangaa kuwa nyumba zao zimebomolewa bila wananchi kupewa ‘notes’.

“Huu ni unyama wa hali ya juu,hatukupewa notes isipokuwa walikuja watu wa Mvomero na kuanza kuweka X na baada ya hapo kesho yake alifajiri nyumba zetu zikaanza kubomolewa, Magufuli alisema tutamkumbuka sasa kweli tunamkumbuka” alisema Manyanda.

Manyanda alisema inashangaza kuona nyumba zao zinabomelewa na wakati uongozi wa mkoa haukuwahi kukutana na wananchi na kuwasikiliza kwani wapo wenye nyaraka za kuwaruhusu kujenga na pia anashangaa kuona nyumba za watumishi wa serikali wakiwemo maaskari nyumba zao hazikuguswa.

Aidha, katika hali isiyo ya kawaida wananchi hao walisikitishwa sana na kitendo cha jeshi la polisi wakiongozwa na Mkuu wa polisi wilaya ya Mvomero kuwazuia waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali kupiga picha wakati zoezi la kubomoa nyumba likiendelea huku wakiwanyang’anya vifaa vyao vya kazi.

Abood anena 

Wakati zoezi la ubomoaji likiendelea kufanyika Mbunge wa Morogoro Mjini Abdulaziz Abood (CCM) alifika katika eneo hilo kwa lengo la kuwajulia hali waliopatwa na kadhia hiyo ambapo alisitisha ubomoaji huo na kuwaomba wananchi kuwa watulivu.

Kamishna wa ardhi Morogoro

Kwa upande wake Kamishna msaidizi wa ardhi Morogoro Frank Minzikuntwe alisema kuwa serikali imesikia ushauri wa Abood na kwamba zoezi hilo lilikuwa likihusu nyumba ambazo zimejengwa baada ya uhakiki kufanyika na siyo vinginevyo.

“Naomba nieleweke tulichokuwa tukifanya ni kubomoa nyumba ambazo watu wamejenga baada ya zoezi la uhakiki kufanyika,hatugusi nyumba ya mtu ambayo ilihakikiwa ambaye yupo upande wa ekari 5113 kama yalivyo maagizo ya serikali” alisema Minzikuntwe.

Mkuu wa wilaya ya Mvomero, Halma Okach mbali na kuhushudia waandishi wa habari wakizuiliwa kuchukua picha alisema kuwa serikali imetumia ustaarabu kuzungumza na wananchi hao lakini wamekuwa wagumu kuelewa na kwamba serikali haipaswi kulaumiwa kwa hilo.

Mkuu wa mkoa wa Morogoro

Baada ya wananchi wa Mtaa wa CCT kuangua vilio kwa masikitiko ya kubomolewa nyumba zao, Mkuu wa mkoa huo Fatma Mwassa amejitokeza na kusema suala hilo liliamuliwa muda mrefu na kilichokuwa kikisubiriwa ni utekelezaji wa zoezi lenyewe ambapo alieleza yeye hapaswi kulaumiwa kwa hilo kwani anatekeleza maagizo ya serikali kwa mujibu wa sheria na siyo vinginevyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

200 wapimwa afya na GGML katika maonesho ya OSHA

Spread the loveZAIDI ya watu 200 jijini Arusha wamejitokeza kupimwa afya na...

Habari Mchanganyiko

Mfanyakazi CRDB atoa sababu za kubambikiwa kesi, hukumu Mei 30

Spread the love  MFANYAKAZI wa Benki ya CRDB, Ibrahim Masahi (40) ameieleza...

Habari Mchanganyiko

Waziri Ummy atangaza Tanzania kuwa kitovu cha utalii tiba

Spread the loveSERIKALI imesema imedhamiria kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha matibabu ya...

Habari Mchanganyiko

Shahidi aeleza namna Nathwani alivyomjeruhi jirani yake

Spread the loveMSIMAMIZI wa Msikiti wa Wahindi Lohana aitwae, Ankit Dawda (32)...

error: Content is protected !!