Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Benki ya Equity yaadhimisha siku ya kimataifa ya wanawake kidigitali
Habari Mchanganyiko

Benki ya Equity yaadhimisha siku ya kimataifa ya wanawake kidigitali

Spread the love

BENKI ya Equity imeadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake kwa kubainisha vipaumbele vya vinavyotoa suluhisho kidigitali katika utoaji huduma za benki kwa wanawake. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Hatua hiyo inalenga kuenda sambamba na kauli mbiu yam waka huu katika maadhimisho hayo ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake inayosema; “Ubunifu na Teknolojia zinatumika kufikia Usawa wa Kijinsia”.

Akizungumzia siku hiyo Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Equity(T), Esther Kitoka amesema mapema mwaka huu, Benki hiyo ilizindua kampeni yao mpya iliyoitwa “tumerahisisha” kwa lengo la kuwafanya wateja wapate huduma za benki za kidigitali kwa urahisi zaidi.

Amesema ili kurahisisha huduma za benki kwa wanawake, wameanzisha mikopo ya kidigitali ambayo inaondoa haja ya kwenda benki ana kwa ana kuonana na maofisa mikopo ili kupatiwa mikopo.

Amesema wamiliki wa akaunti za kikundi pia wanaweza sasa kupata huduma zao kupitia simu zao za mkononi.

Aidha, amesema wanatoa mikopo ya kilimo kusaidia wanawake katika kuboresha kilimo chao na kugeuza kuwa biashara yenye faida ili kujiunga kiuchumi.

Amesema Siku ya Kimataifa ya Wanawake ni maadhimisho ya mafanikio ya kijamii, kiuchumi, kitamaduni na kisiasa ya wanawake, pamoja na wito wa kuchukua hatua za kuongeza kasi ya usawa wa kijinsia.

“Faida za usawa wa kijinsia sio tu kwa wanawake na wasichana bali kwa kila mtu ambaye maisha yake yatabadilika kutokana na dunia yenye usawa.

“Mwaka huu, lengo kuu ni kusherehekea wanawake na wasichana ambao wamebadilisha teknolojia katika sekta mbalimbali, ikiwemo benki, kote ulimwenguni,” amesema.

Amesema Benki ya Equity iko mstari wa mbele katika mapambano ya kuhakikisha huduma zao zote zinatolewa kidigitali.

“Tunajivunia kuwa na Mkurugenzi Mtendaji mwanamke, Isabela Maganga ambayo ni hatua kubwa kwetu kama taasisi kuonyesha kwamba wanawake wanaweza kuongoza kwa mifano halisi.

“Ni muhimu kuendelea kupigania usawa wa kijinsia wenye manufaa. Kwa muda mrefu, wanawake wameachwa nyuma katika ushiriki wa teknolojia. Tunapaswa kuongeza ushiriki wa wanawake katika teknolojia kwa sababu maendeleo hayawezi kutenganishwa na teknolojia,” amesema.

Amesema Benki ya Equity inaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake siyo tu kwa kutambua mafanikio ya wanawake bali pia kwa kutoa elimu ya kidigitali kwenye majukwaa mbalimbali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yatoa elimu matumizi sahihi ya zebaki kwa wachimbaji

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

error: Content is protected !!