Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Lwaitama: Wakati wa Magufuli ungeweza kutagazwa mbunge hata kama hujachaguliwa
Habari za Siasa

Dk. Lwaitama: Wakati wa Magufuli ungeweza kutagazwa mbunge hata kama hujachaguliwa

Spread the love

UTEUZI wa wabunge wa viti maalum 19 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wakiongozwa na Halima Mdee, umeibua mvutano wakati Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la chama hicho, Dk. Azavel Lwaitama, akihojiwa katika Mahakama Kuu,

Masjala Kuu, jijini Dar es Salaam ambapo ameeleza kuwa wakati wa utawala wa Dk. John Magufuli mtu aliweza kutangazwa kuwa mbunge hata kama hakuchaguliwa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mvutano huo umeibuka leo Alhamisi tarehe 9 Machi 2023, wakati Dk. Lwaitama akiulizwa maswali ya dodoso na Wakili wa wabunge hao, Ipilinga Panya, mbele ya Jaji Cylrian Mkeha.

Ni katika kesi Na. 36/2022, iliyofunguliwa na wabunge hao kupinga uamuzi wa Chadema kuwavua uanachama kwa madai kwamba ulikuwa kinyume cha sheria.

Mjadala huo uliibuka baada ya Wakili Panya, kumhoji Dk. Lwaitama kama anawatambua wabunge hao, ambapo alijibu akidai kwamba anawafahamu.

Wakili Panya alimhoji Dk. Lwaitama wabunge hao ni kina nani, ambapo alijibu akidai kwamba wamefukuzwa.

Mvutano huo ulishika kasi zaidi baada ya Wakili Panya kumhoji wabunge hao waliapa kuwa nani? Ambapo majibizano yao yalikuwa kama ifuatavyo;

Wakili Panya: Waliapa kuwa nani?

Dk. Lwaitama: Waliapishwa na Ndugai

Wakili Panya: Kuwa nani?

Dk. Lwaitama: Hiyo ndiyo ilikuwa taharuki sababu mamlaka yao haikuwaambia….

Wakiki Panya: Waliapishwa kuwa nani?

Dk. Lwaitama: Waliapishwa kuitwa wabunge

Wakili Panya: Hivi waliapishwa au hawakuapishwa?

Dk. Lwaitama: Hawa viti maalum majina yao yalipelekwa na mamlaka zao hawajafanya hivyo na hii ilikuwa wakati wa Magufuli

Wakili Panya: Nani mwenye mamlaka ya kumtangaza mtu mbunge viti maalum?

Dk. Lwaitama: Nchi hii wakati wa Magufuli unaweza ukatangazwa hata kama hujachaguliwa.

Wakili Panya: Utaratibu wa uteuzi ndani ya chama uliendaje?

Dk. Lwaitama: Taratibu za kupelekwa majina hazikufuatwa na sisi wanachama tulipata taharuki waliendaje na ndicho nilichosema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!