Spread the love

SERIKALI imesema kuwa bado watanzania wanakabiliwa na hali ya umasikini hivyo kuna kila sababu ya taasisi za kifedha kutoa elemu. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Hayo yameelezwa leo  tarehe 09 Julai 2019, wakati Benki ya TPB  ikikabidhi gawio la Sh. 1.2 bilioni kwa Serikali ya Tanzania pamoja na Wanahisa wengine wa benki hiyo.

Gawio hilo limetokana na faida ambayo benki hiyo imeipata kutokana na shughuli zake katika kipindi cha mwaka 2017/18.

Akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi gawio hilo iliyofanyika kwenye ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango mjini Dodoma, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya TPB, Dk. Edmund Mndolwa amesema  benki ya TPB imefanya vizuri mwaka jana kwa kupata faida ya Sh.  17 bilioni na hivyo kuweza kutoa gawio la Sh. 1 bilioni na Sh. 1.2 bilioni kwa Serikali pamoja na Wanahisa wake.

“Mimi kama Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya TPB najisikia faraja kusimamia benki inayoendelea kufanya vizuri miongoni mwa mabenki takriban 54 yaliyopo sokoni hivi sasa.

“Wanahisa wanaridhishwa na utendaji wa benki kwa kipindi hicho kwani benki ilifanikiwa kupata faida ya kiasi cha shilingi bilioni 17.2 kabla ya kodi.

“Nichukue fursa hii kuwashukuru sana wateja wetu ambao wameendelea kutuamini kwa kutumia huduma zetu kwa wingi.

“Ahadi yetu kwao ni kwamba tutaendelea kutoa huduma bora na zenye kukidhi mahitaji yao,” alisema Dk. Mndolwa

Akipokea gawio hilo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango amesema kuwa watanzania bado ni masimini kutokana na kutokujua au kutokuwa na elimu ya nidhamu ya fedha.

Licha ya kutaka mabenki kutakiwa kutoa elimu kwa watanzania kupewa elimu ya nidhamu ya fedha ameipongeza  benki ya TPB kwa kuendelea kufanya vizuri miongoni mwa mabenki takriban 50 yaliyopo nchini.

“Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa uongozi wa Benki ya TPB kwa gawio hili la shilingi Bilioni Moja mlilolitoa kwa Serikali.

“Hii ni mara ya  pili mfululizo kwa benki hii kufanya hivyo, na kwa sababu hiyo basi, nitoe pongezi kubwa na za dhati kwa uongozi wa TPB kwa gawio hili. Kutoa kwenu gawio kwa wanahisa wenu kunaashiria kwamba Benki ya TPB imeendelea kufanya vizuri kiutendaji, na hii inatia moyo na kutoa hamasa kwa wanahisa tunaomiliki hisa kwenya benki yenu.

“Hii ni ishara pia kuwa taasisi zinazomilikiwa na Serikali zinaweza kujiendesha kwa ufanisi na kwa faida, kiasi cha kuweza kutoa ushindani kwa taasisi nyingine za binafsi,” amesema Dk. Waziri Mpango.

Waziri Dk. Mpango pia alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa taasisi za Serikali kutumia huduma za kibenki kutoka benki hiyo kupitia matawi yake yaliyoenea nchi nzima ili kuiunga mkono.

“Napenda kutoa wito kwa taasisi zingine za umma zinazotaka huduma za Kibenki kote nchini Tanzania na Watanzania wote kwa ujumla kutumia huduma za Benki ya TPB zilizoko mikoa yote nchini Tanzania.

Benki ya TPB yenye matawi 75 nchi nzima inao wanahisa sita ambao ni   Serikari ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Shirika la Posta, Saccos ya Posta na Simu, Workers Compensation Fund pamoja na PSSSF.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *