Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Msiba wa wafanyakazi Azam watikisa, mwendokasi wapigiwa kelele
Habari MchanganyikoTangulizi

Msiba wa wafanyakazi Azam watikisa, mwendokasi wapigiwa kelele

Spread the love

VIONGOZI  mbalimbali wa kisiasa na watu mashughuli wametao neno la pole kwenye msiba wa wafanyakazi watano wa Azam TV  waliofariki jana kwenye ajali  mkoani Singida. Anaripoti Faki Sosi …(endelea).

Wafanyakazi hao ni Saidi Haji, Salim Mhando, Florence Ndibalema, Sylvanus Kasongo na Charles Wandwi, waliokuwa njiani kuelekea Chato kwenye uzinduzi wa  Hifadhi ya Taifa  ya Burigi inayozinduliwa leo na Rais Magufuli.

Watu hao mashughuli na viongozi wa kisiasa wamehudhuria kwenye Ofisi za Azam Media kwa ajili ya kuaga na kuwafariji wafiwa na wafanyakazi wenzao marehemu.

Freeman Mbowe Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amesema kuwa msiba huo umegusa taifa na kipekee chama hicho kimeguswa na msiba huo kwa namna walivyokuwa wakishirikiana na wafanyakazi hao.

Amesema kuwa taifa letu lijikumbushe kuwa vyombo vya habari vinaumuhimu wa kuijenga au kiubomoa nchi.

Profesa Ibrahim Lipumba Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), amesema kuwa msiba huo  ni pengo na chama hiko pia kimekuwa kikifanya kazi kwa ukaribu na wafanyakazi hao.

Januari Makamba Waziri wa Ofisi Makamo wa Rais Muungano na Mazingira ameeleeza kifo hiko kuwa ni pengo kwa taifa na Tasnia ya habari.

Humphrey Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenezi ameeleza hisia zake juu ya msiba huo na kwamba  alikuwa akiwajua wafanyakazi hao mmoja mmoja kutokana na kufanyakazi kwa ushirikiano.

Joyce Mhavile wa ITV na Radio One ameeleza kuwa yanayotokea yanasikitisha lakini ni wajibu wa kila mwanadamu.

Ayoub Rioba, Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) licha ya kupoteza vijana hao wachapakazi lakini ndio uhalisia wa maisha.

Deodatus Balile, Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), ametoa pole kwa familia na wanahabari.  “Matukio kama haya tunapaswa kujiuliza picha za tukio hilo zinaonekana kuwa ni mwendokasi wakati tunaaga wenzetu tutafakari mwendo wetu barabarani.”

Amesema kuwa wamiliki wa vyombo vya moto kuwa makini kwenye uendeshaji wa vyombo hivyo wakiwa barabarani.

Rose Roben, mwakilishi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), amesisitiza umakini kwa watumiaji wa vyombo vya moto wakiwa barabarani.

Tully Mwambapa, Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, amesema wanatoa pole kwa familia za marehemu na kutoa pole ya Sh. 1 milioni kwa kila familia.

Wilfred Kidau, Katibu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania  (TFF), amesema kuwa shirikisho hilo limepata pigo kwa kutokana na msiba  huo kwani wamekuwa wakifanya kazi pamoja na Azam kupitia Ligi Kuu Tanzania Bara.

Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, amesema kuwa neno shukrani haliwezi kuponya kuwakumbusha watu  kwamba tukumbuke kuwa uhai ni zawadi.

Hamadi Masauni, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani amesema kuwa kifo hiko kimeligusa taifa na kwamba serikali imefanya uchunguzi ajali hiyo  na inakaribia kupata chanzo chake ili kuepusha tukio jengine. Amewataka wananchi kuzitii sheria za barabarani na za nchi kwa ujumla.

Tido Muhando, Mkurugenzi  wa Azam Media amesema kuwa  msiba huo umemstua kutokana na mazingira yake.

Anasema kuwa vijana hao wachapakazi na wanajitoa kwenye kazi na kwamba  vijana hao waliondoka kuelekea wilayani Chato kwa kujichagua wenye ilhali ilikuwa siku ya Jumapili na yenye mapumziko.

Ameleeza kwa namna watu walivyojitokeza kwa wingi kumewafariji wafanyakazi wa Azam na kitendo hiko kitawaongezea ari ya kuwatumikia Watanzania.

Haji Manara, Msemaji wa Simba licha kukumbuka namna watu hao wakirusdha mechi za mpira mubashara amesema kuwa klabu ya Simba imefanya kazi kwa ukaribu na wafanyakazi hao.

Dismas Ten, Msemaji wa Klabu ya Yanga amesema kuwa klabu hiyo imefanya kazi na Azam kama taasisi mbili zenye mshikamano.

Wengine waliohudhuria kwenye kutoa heshima kwa wafanyakazi hao eneo Tabata  kwenye Ofisi za Azam TV, ni pamoja na Zitto Kabwe Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Balozi Hamis Kagasheki, Suleiman Khalifa, Katibu Mkuu wa Chama CUF, Lazaro Mambosasa, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,  Francis Ciza (Majizo), Mmiliki wa TV E na EFM, Jerry Muro, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mgaya Kingoba, Mhariri wa Magazeti ya TSN,

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

error: Content is protected !!