Wednesday , 8 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Mfumuko wa bei wazidi kupaa
Habari Mchanganyiko

Mfumuko wa bei wazidi kupaa

Spread the love
MFUMUKO wa bei wa taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Juni ,2019 umeongezeka hadi kufikia  asilimia 3.7 kutoka asilimia 3.5 kwa mwaka ulioishia mwezi Mei 2019. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Hayo yamesemwa leo jijini hapa na Mkurugenzi wa takwimu za uchumi ,Ofisi ya taifa ta takwimu, Daniel Masolwa wakati akitoa taarifa ya mfumko wa bei wa mwezi unaopima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi nchini.

Akitoa taarifa hiyo Masolwa alisema mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Juni, 2019 imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2019.

Pamoja na hayo Mkurugenzi huyo alisema kuongezeka kwa mfumuko huo kumechangiwa na kuongezeka kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula kwa kipindi cha mwaka ulioishia mwezi Juni, 2019 zikilinganishwa na bei za mwaka ulioishia mwezi Juni 2018.

“Baadhi ya bidhaa za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa mfumuko wa bei wa mwezi Juni 2019 ni pamoja na unga wa mahindi kwa asilimia 3.6, samaki wabichi asilimia 27.3, unga wa ngano kwa asilimia 4.4 na mtama kwa asilimia 4.9,” alisema Masolwa.

Aidha alizitaja bidhaa zisizo za chakula zilizochangia kuongezeka kwa mfumuko wa bei wa mwezi Juni 2019 kuwa ni pamona na dizeli kwa asilimia 11.4, petroli kwa asilimia 4.9, gharama za kulala kwenye nyumba za wageni kwa asilimia 5.8 na vitabu vya shule kwa asilimia 2.4.

Pamoja na mambo mengine, Mkurugenzi huyo  wa takwimu za uchumi aliongeza kuwa mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwaka ulioishia mwezi Juni 2019 umeongezeka hadi kufikia asilimia 2.3 kutoka asilimia 2.2 kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2019.

“Hata hivyo kwa hali ya mfumuko wa bei kwa nchi za Afrika mashariki kwa mwaka ulioishia mwezi Juni, 2019 nchini Uganda umeongezeka hadi asilimia 3.4kutoka asilimia 3.3,” alisema.

Pamoja na hayo alisema,kwa upande wa Kenya mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Juni, 2019 umeongezeka hadi asilimia 5.70 kutoka asilimia 5.49 kwa mwaka ulioishia mwezi Mei 2019

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mawakili waiburuza mahakamani TLS, EALS

Spread the love  WAKILI Hekima Mwasipu na wenzake wawili, wamefungua kesi katika...

Habari Mchanganyiko

Uvuvi bahari kuu wapaisha pato la Taifa

Spread the love  SERIKALI imesema uvuvi wa bahari kuu umeliingizia Taifa pato...

Habari Mchanganyiko

DPP aweka pingamizi kesi ya ‘watu wasiojulikana’

Spread the love  MKURUGENZI wa Mashtaka nchini (DPP), ameweka pingamizi dhidi ya...

Habari Mchanganyiko

Washindi saba safarini Dubai NMB MastaBata ‘Kote Kote’

Spread the loveKAMPENI ya kuhamasisha matumizi ya Mastercard na QR Code ‘Lipa...

error: Content is protected !!