NI kama maneno ya kumnadi Mwita Waitara yamewaishia makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kwanza kushambulia rangi za bendera ya Chadema. Anaandika Mwandishi Wetu … (endelea).
Livingstone Lusinde, Mbunge wa Mtera kupitia CCM ameishambulia rangi nyekundu iliyopo kwenye bendera hiyo akihoji maana yake.
Lusinde ametoa kauli hiyo leo tarehe 13 Septemba wakati wa kumnadi Waitara katika uchaguzi mdogo unaotarajia kufanyika tarehe 16 Septemba mwaka huu kwenye Jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam.
Lusinde amedai kuwa rangi nyekundu kwenye bendera ya Chadema haina uhalisia na kwamba rangi ya kijani ya CCM ina maana halisi.
“Mnawekaje bendera nyekundu, mlipigana vita wapi? Likipita gari la mzigo linaweka bendera nyekundu kwamba mzigo umezidi bodi sasa Chadema mzigo umezidi bodi vijana shukeni,” amesema.
Kwenye mkutano huo Lusinde amesema, Waitara anajua shida za wana Ukonga hivyo amewaomba wamchague ili ashirikiane na CCM kuzitatua.
Hata hivyo amesema, Waitara sio Mungu na hawezi kuzitatua zote kwani mwenye uwezo wa kutatua matatizo yote ni Mungu pekee.
Leave a comment