Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe, Lowassa wala kiapo Monduli
Habari za SiasaTangulizi

Mbowe, Lowassa wala kiapo Monduli

Spread the love

FREEMAN Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema Taifa na Edward Lowassa, Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho wameapa hadharani kumkabili Rais John Magufuli. Anaripoti Mwandishi Wetu, Monduli … (endelea).

Viongozi hao wa Chadema wameeleza kuchoka kuvumilia kile walichokiita uvunjifu wa haki na Uhuru na sasa wamepanga ‘kulianzisha’ baada ya uchaguzi huu mdogo.

Wamesema kuwa, pamoja na Katiba ya Tanzania kuelezea Uhuru na haki kama mambo ya msingi kwa Watanzania bado vimekuwa vikiminywa na utawala wa sasa wa Rais John Magufuli.

Viongozi hao wametoa kauli hiyo tarehe 13 Septemba mwaka huu mbele ya wakazi wa Monduli wakati wa kumnadi Yonas Leizer anayegombea ubunge kupitia wa Jimbo la Monduli Chadema.

Kwenye mkutano huo Lowassa amesema, hali ilivyo si ya kuvumilika na kwamba anatamani angekuwa na nafasi ya kugombea ubunge ili akasimamie Uhuru na haki bungeni.

Lowassa amesema kwamba, yanayotokea kwa sasa yanaweza kudhibitiwa kwa kupatikana Katiba Mpya.

“Katiba Mpya inatakiwa ili kumtoa adhabu kwa kila atakayekwenda kinyume ikiwa ni pamoja na kuzuia mikutano ya hadhara, bunge, kuzuia wapinzani kushika madarana,” amesema.

Mbowe amesema kuwa pamoja na Rais kuapa kwa kutumia kitabu cha imani yake lakini huapa kuilinda Katiba ya nchi.

“Tunapaswa kujua kwamba hakuna aliye juu ya sheria si kwa rais wala mtawaliwa,” amesema Mbowe.

Amesema kuwa, baada ya uchaguzi huu mdogo wamepanga kuanza kusaka Uhuru na haki kwa Watanzania wote na watasimamia hilo.

Katika mkutano huo Mbowe ameeleza kushangazwa na CCM kutumia viongozi wa serikali wakiwa na magari ya serikali jambo ambalo ni kinyume na sheria.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

error: Content is protected !!