Saturday , 2 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa BAVICHA wamgeuzia kibao Sembeye
Habari za Siasa

BAVICHA wamgeuzia kibao Sembeye

Nusrat Hanje, Katibu wa BAVICHA
Spread the love

BARAZA la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA), limemtaka Edward Sembeye, aliyekuwa Mratibu wa Uhamasishaji wa baraza hilo kueleza ukweli kilichomkimbiza Chadema. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Wito huo umetolewa jana tarehe 26 Februari 2020, na Nusrat Hanje, Katibu wa BAVICHA wakati akitoa ufafanuzi kuhusu tuhuma zilizotolewa na Sembeye alipotangaza kukihama chama hicho, jana jijini Dar es Salaam.

Hanje amesema Sembeye hajaondoka Chadema kwa sababu ya chama hicho kuwa mali ya mtu mmoja, bali amechukua hatua hiyo kutokana na hasira ya kukosa nafasi aliyotaka ndani ya chama hicho.

“Sisi vijana wa nchi hii hasa wa Chadema  lazima tuwe wakweli tunapozungumza, sio dhambi mtu kuhama chama kimoja kwenda kingine lakini tudiriki kusema kweli kwa nini umehama, Sembeye anajulikana  alihama kwa sababu alitaka kugombea nafasi akaikosa hakuipata amehama kwa hasira, pamoja na kwamba amemfuata katibu mkuu aliyeenda CCM,” amesema Sembeye.

Aidha, Hanje amesema Sembeye hakuwa katibu wa BAVICHA kama alivyojitambulisha kwa wanahabari, bali alikuwa mgombea wa nafasi hiyo katika uchaguzi uliofanyika mwaka 2019, kutokana na kuwa na umri mkubwa.

“Kuna mtu anaitwa Edward Sembeye aliwahi kuwa mratibu wa uhamasishaji BAVICHA Taifa uongozi wa 2014-19 lakini mwaka 2019 aligombe ana mimi hapa niligombea nae lakini umri wake ulikuwa umezidi aliondolewa kwa sababu alikiuka utaratibuw a chama wa ndani ya chama mtu akitaka kugombea anatakiwa kuwa umri unaotakiwa,” amesema Hanje na kuongeza:

“ Mimi ndio katibu mkuu wa vijana na kama kwa namna yoyote alidanganya watu kama katibu mkuu wa vijana naomba maelezo yake yapuuzwe sababu yeye alikuwa mgombea wa nafasi ya ukatibu mkuu wa vijana sio katibu.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia kuzindua programu ya nishati safi ya kupikia kwa wanawake Afrika

Spread the loveRais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua programu ya...

Habari za Siasa

AG aiagiza kamati ya maadili kuwashughulikia mawakili wanaokiuka maadili

Spread the loveMWANASHERIA Mkuu wa Serikali (AG), Dk. Eliezer Feleshi, ameagiza Kamati...

Habari za Siasa

Jaji avunja ukimya sakata la Mpoki kusimamishwa uwakili

Spread the loveJAJI Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma, amekitaka Chama cha...

Habari za Siasa

Sheikh Ponda ataka mwarobaini changamoto uchaguzi 2020

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa...

error: Content is protected !!