April 12, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Hofu ya Corona: Saud Arabia yazuia Ibada ya Umra

Spread the love

IBADA ya Umra inayotekelezwa na Waislamu nchini Saud Arabia, imezuiwa kwa muda kutokana na hofu ya kusambaa kwa virusi vya Corona. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Ibada ya Umra hufanyika wakati wowote tofauti na Ibada ya Hijja ambayo hujumuisha mamilioni ya watu kutoka mataifa yote dunaini, huwekwa muda maalumu.

Kutokana na kusambaa kwa virusi hiyo katika mataifa mbalimbali sasa, vikianzia taifa la China, serikali ya Saudia imefikia uamuzi huo ikiwa ni hatua ya awali katika kuchukua tahadhari kwa taifa hilo lakini pia kuepuka kusambaza kwa watu wataporudi kwao baada ya ibada hiyo.

Licha ya Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo kueleza, marufuku hiyo ni ya muda lakini mpaka sasa haijajulikana kama katazo hilo litakoma lini.

Upo wasiwasi kwamba, kulingana na mazingira hayo upo uwezekano katazo hilo likaathiri ibada ya Hijja inayotarajiwa kuabza kutekelezwa mwishoni mwa Julai mwaka huu, na ambayo huhusisha mkusanyiko mkubwa zaidi wa watu duniani.

Katika kujihami na virusi vya Corona, Saudi Arabia imepiga marufuku watu kutoka mataifa yaliyokumbwa na virusi hivyo kuingia nchini humo.

Mpaka sasa, zaidi ya watu 2,700 wamefariki dunia kutokana na ugonjwa huo.

error: Content is protected !!