April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Vitabu vipya Shule za Msingi, Sekondari vyazinduliwa

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wiliam Tate Ole Nasha akizindua vitabu vya kiada kwa shule zinazotumia lugha ya Kingereza, pamoja na vitabu vya wanafunzi wenye mahitaji maalumu.

Spread the love

CHANGAMOTO ya uhaba wa vitabu vya kiada kwa shule zinazotumia lugha ya Kingereza, pamoja na vitabu vya wanafunzi wenye mahitaji maalumu, imepatiwa mwarobaini wake. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Leo tarehe 27 Februari 2020, jijini Dar es Salaam, serikali kupitia Taasisi ya Elimu nchini (TET), imezindua aina sita ya vitabu vya kiada vya Darasa la Kwanza na Pili, vitabu vya kiada vya Darasa la Nne na Tano kwa shule zinazotumia Kingereza, pamoja na vitabu vya maandishi ya nukta nundu vya Kidato cha Kwanza hadi Nne.

Akizungumza kuhusu uzinduzi huo, William Tate Olenasha, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, amesema upatikanaji wa vitabu hivyo utamaliza changamoto ya uhaba wa vifaa vya kufundishia kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu nchini, ambao kwa muda mrefu walishindwa kupata elimu bora.

“Leo hii ukiacha kutatua changamoto za watoto wenye mahitaji maalumu. Tumetatua changamoto ya watoto wa Watanzania wanaosoma shule za English Medium,  ambao kwa muda mrefu walikuwa wanatumia vya lugha za kiswahili. Lengo ni kuhakikisha elimu inawafikia watoto wote bila kujali tofauti zao,” amesema Olenasha.

Olenasha ameagiza halamshauri zote nchi kuhakikisha zinasambaza vitabu hivyo shuleni, huku akiwataka wamili wa shule binafsi kuwasiliana na TET kwa ajili ya kupata njia sahihi ya kununua vitabu hivyo.

“Kama wamiliki wanapata tabu ya kupata, wafanye mawasiliano ya ofisi ya kanda au ofisi ya TET maana vipo,  vinapatikana kwa urahisi unalipia gharama za uchapishaji. Hivi sio vya biashara,” amesema Olenasha na kuongeza:.

“Wasimamizi wote wapeleke vitabu shuleni kwa haraka. Rai yangu ni kwmba wakurugenzi TAMISEMI hakikisheni vinasambazwa haraka. Na jukumu la kusambaza ni halamshauri husika, hakikisheni vinafika kwa wakati ili viendelee kutumika.”

error: Content is protected !!