Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Michezo Azam FC yapata kocha mpya, apewa mwaka 1
Michezo

Azam FC yapata kocha mpya, apewa mwaka 1

Spread the love

MATAJIRI wa jiji la Dar es Salaam kutoka  Chamazi – Timu ya soka ya Azam FC baada ya kuanza msimu mpya wa Ligi Kuu Bara kwa kusuasua wamemleta kocha mwenye mpya, Denis Lavagne kutoka nchini Ufaransa anayenasibiwa kulijua zaidi Soka la Afrika.  Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kocha huyo raia wa Ufaransa, mwenye wasifu mkubwa, akiwa na leseni ya juu ya ukocha (UEFA Pro Licence), anakuja kuchukua mikoba ya Abdihamid Moallin.

Lavagne ametua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na kupokelewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Azami, Abdulkari Amin.

Kwa mujibu wa msemaji wa Klabu hiyo, Zakaria Thabith ‘Zaka za Kazi’, amesema ZaLavagne ambaye amewasili nchini leo Jumanne, amepewa mkataba wa mwaka mmoja tayari kuanza rasmi majukumu yake hayo.

Mfaransa huyo, ni kocha aliyewahi kufundisha timu ya Taifa ya Cameroon (2011-2012), miamba ya Algeria, USM Alger na JS Kabylie.

Aidha, amewahi kufundisha vigogo wa Tunisia, Etoile Du Sahel (2013), Smouha ya Misri, Coton Sports (Cameroon), Al Hilal ya Sudan.

Moja ya mafanikio yake ni kufika fainali ya michuano ya Lugi ya Mabingwa Afrika mwaka 2008 akiwa na Coton Sport ya Cameroon na kupoteza dhidi ya Al Ahly ya Misri kwa jumla ya mabao 4-2.

Ubora wa mbinu zake, zilimwezesha mwaka jana, kuiongoza JS Kabylie ya Algeria kushika nafasi ya pili kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, ikicheza fainali na Raja Casablanca ya Morocco na kupoteza kwa mabao 2-1.

Mtaalamu huyo anatajwa kuwa kocha wa makombe, kwani aliiwezesha Coton Sport kutwaa mataji manne ya ligi (2007, 2008, 2010, 2011), aliiongoza Al Hilal kutwaa taji la ligi mwaka 2016, aliiongoza JS Kabylie kubeba taji la Kombe la FA (2021) na Etoile Du Sahel kutwaa ubingwa kama huo Tunisia mwaka 2013.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Europa na Conference kukupatia pesa ndefu leo

Spread the love  ALHAMISI ya leo tutaenda kushuhudia mitanange ya kukata na...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

Michezo

Usiku wa Ulaya umerejea kibabe kabisa

Spread the love  LIGI ya Mabingwa barani Ulaya imerejea tena na awamu...

Habari MchanganyikoMichezo

Mambo ya Ndani, Ulinzi zang’ara michezo ya Mei Mosi Arusha

Spread the loveRais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Tumaini...

error: Content is protected !!