Friday , 17 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Makamba amuwakilishi Samia mkutano mabadiliko tabia nchi Afrika
Habari Mchanganyiko

Makamba amuwakilishi Samia mkutano mabadiliko tabia nchi Afrika

Spread the love

WAZIRI wa Nishati, Januari Makamba amemwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano wa Viongozi wa Dunia unaojadili Program ya Afrika ya kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Africa Adaptation Summit) unaofanyika Rotterdam, Uholanzi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mkutano huo uliofanyika jana tarehe 5 Septemba, 2022, unalenga kushawishi Washirika wa Maendeleo, Taasisi za Kifedha na Sekta binafsi na marafiki wa Afrika kuchangia fedha kwenye Programu hiyo ya Afrika ambayo inahitaji Dola za Marekani Bilioni 25 ifikapo 2025. Benki ya Maendeleo ya Afrika imechangia Dola za Marekani bilioni 12.5.

Mkutano huu unafanyika kama sehemu ya maandalizi mkutano wa 27 nchi wananchama wa mkataba wa  mabadiliko ya Tabia Nchi ambao unatarajiwa kufanyika mwezi Novemba  mwaka huu huko Sharm El  Sheik Mistri ambako suala la kuhimili mabadiko ya Tabia Nchi kwa Afrika ni moja ya agenda muhimu ya mkutano huo.

Katika Mkutano Waziri wa Nishati amekutana na Viongozi wa Dunia, Wakuu wa Taasisi na Mashirika mbalimbali na kujadiliana nao fursa mbalimbali ikiwa pamoja na namna bora ya Tanzania kunufaika na Mpango huo wa AFRICA ADAPTATION ACCELERATION PROGRAM (AAAP) ambao utaharakisha mipango ya nchi katika kukabiliana na majanga yakiwemo UVIKO19, ukame, njaa, ajira kwa vijana na mafuriko.

Mkutano huo uliongozwa na Rais Senegal na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika pamoja Macky Sally na Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa pia Mwenyekiti wa Kituo cha kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (GCA), Ban Ki-Moon.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari Mchanganyiko

Wananchi washauriwa kuongeza uelewa wa kujikinga na majanga

Spread the love WITO umetolewa kwa wananchi kuongeza uelewa na utayari kabla...

error: Content is protected !!