Sunday , 28 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Anusurika kifo kwa kushambuliwa na wanawake waliokuwa wanaondoa mikosi
Habari Mchanganyiko

Anusurika kifo kwa kushambuliwa na wanawake waliokuwa wanaondoa mikosi

Spread the love

 

KAMANDA wa Jeshi la Polisi mkoani Simiyu, ACP Blasius Chatanda, amesema mwanaume mmoja ambaye hakumtaja jina, amenusurika kifo baada ya kushambuliwa kwa mawe na kundi la wanawake zaidi ya 50, waliokuwa wanaondoa mikosi baada ya mwenzao kupoteza mtoto wakati anajifungua. Anaripoti Mwandishi Wetu, Simiyu … (endelea).

Akizungumza na wanahabari leo Jumamosi, tarehe 18 Desemba 2021 mkoani Simiyu, ACP Chatanda amesema tukio hilo lilitokea tarehe 9 Desemba mwaka huu, baada ya wanawake hao kumshambulia mwanaume huyo, ambaye ni mkandarasi anayetengeza barabara kutoka Bariadi kwenda Kata ya Nkololo mkoani humo.

“Tarehe 9 Desemba 2021, muda wa asubuhi maeneo ya Kijiji cha Nkololo, Wilaya ya Bariadi, bwana mmoja mhandisi alishambuliwa na wanawake waliokuwa kwenye kundi waliokuwa zaidi ya 50, kwa mawe, katika maeneo mbalimbali ya mwili wake na kumsababishia majeraha,” amesema ACP Chatanda.

ACP Chatanda amesema kuwa, mwanaume huyo alinusurika kifo katika mkasa huo, baada ya kuokolewa na wenzake waliowahi kufika eneo la tukio.

“Kimsingi ni kitu cha kinyama kukutana na mtu barabarani na kumsababishia madhara, vinginevyo yule kama sio msaada wa wenzake wangemuua, nawasihi wenyeji wanaoendekeza mila ya aina hii waachane nayo mara moja,” amesema ACP Chatanda.

ACP Chatanda amesema, chanzo cha tukio hilo ni mila zinazodaiwa za kabila la Wasukuma, zinazoelekeza mama anapofariki dunia wakati anajifungua, au mtoto akifariki dunia wakati anazaliwa, wanawake kufanya tambiko kwa kumpiga mawe mwanaume.

“Kwa mujibu wa taratibu za Kisukuma ni kwamba, mwanamke akiwa mjamzito na mtoto akazaliwa kisha akafariki au mama akafariki wakati wa kujifungua, inatakiwa wenzake waliobakia waondoe mkosi, sasa mkosi huu unaondolewa kwa wao kwenda kwenye eneo ambalo watafanya tambiko,” amesema ACP Chatanda.

ACP Chatanda amesema, kwa bahati mbaya wakati wanawake hao wanarudi katika tambiko hilo, walikutana na mkandarasi huyo kisha wakaanza kumshambulia kwa kumpiga mawe.

 “Na wakitoka kwenye tambiko wanaporudi njiani, basi mwanaume yeyote wanayekutana naye watamshambulia kwa mawe, kama namna ya kutoa mikosi. Siku ya tukio hili huyu mkandarasi alikuwa ameamka kwenda kazini, kwa bahati mbaya na kutokujua kwa kuwa yeye ni mgeni,” amesema ACP Chatanda.

ACP Chatanda amesema “katika eneo hilo  alikutana na kina mama, ambao kwa wakati huo waliona ni mtu sahihi kuondoa mkosi ulitokana na mwenzao aliyepoteza mtoto aliyekuwa anazaliwa. Kufuatia hali hiyo walianza kumshambulia kwa mawe na kumsababishia majeraha hadi hapo alipopata msaada walipokuja wenzake.”

ACP Chatanda amesema, Jeshi la Polisi mkoani humo linawashikilia wanawake nane wakidaiwa kuhusika katika tukio hilo na kwamba watafikishwa mahakamani mara moja, ili sheria ichukue mkondo wake.

“Hawa wote nane tuliowakamata  tutawafikisha mahakamani, ili sheria zichukue mkondo wake na wengine watambue hakuna sababu za kuendekeza mila ambazo zina madhara, kwa jamii inayoishi na watu wengine ambao ni wapitaji sio wenyeji,” amesema ACP Chatanda.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wami Ruvu hawana deni la Rais Samia katika kutunza vyanzo vya maji

Spread the love  BODI ya Maji Bonde la Wami Ruvu, imeendelea kuchua...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari Mchanganyiko

Dk. Jafo aipongeza Oryx kumuunga mkono Samia

Spread the loveWAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na...

Habari Mchanganyiko

Mvungi aendesha kikao kazi cha wataalam wa Regrow

Spread the love  MKURUGENZI wa Idara Sera na Mipango Wizara ya Maliasili...

error: Content is protected !!